Home Kitaifa Chilunda anaondoka lini kwenda Hispania?

Chilunda anaondoka lini kwenda Hispania?

10664
0
SHARE

Chilunda ameshaingia mkataba wa miaka miwili na Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania.

Kilichobaki ni kuondoka kwenda Hispania kuanza maisha mapya, kuhusu anaondoka lini ndio swali ambalo kila mtu angependa kujibiwa maana isijekuwa amesaini mkataba ambao ataanza kuutumikia mwaka ujao.

“Kuhusu suala la kuondoka nasubiri kibali cha kazi kitoke kule (Hispania), wameshakifatilia hakitachukua muda mrefu kitatumwa huku ili nifatilie visa kwa ajili ya kuondoka”-Shabani Chilunda.

“Nimesaini mkataba wa miaka miwili lakini wakati wowote timu ikitokea kunihitaji wataniuza.”

“Ukiifatilia Tenerife ni timu nzuri ambayo inauza wachezaji kwenda timu kubwa lakini ni timu ambayo inafanya vizuri, kwangu mimi ni level kubwa kwa sababu kutoka ligi ya Tanzania hadi  Segunda ni maendeleo makubwa na naamini ntacheza na kupata timu kubwa zaidi ya pale.”

Chilunda anaondoka Azam huku akiamini timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao kutokana na uboreshaji uliofanywa kwenye benchi la ufundi.

“Kila mwalimu ana plan yake, mwalimu kafika kaangalia wachezaji anaowataka anaweza kufanya nao kazi, naamini wachezaji ambao kawasajili mwenyewe atawapa nafasi na watafanya vizuri”

Baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame Cup 2018 Shabani Idd Chilunda ameushukuru Azam kwa kuwa naye kwa kipindi chote walichomlea kama mchezaji.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here