Home Makala Usirudishe rimoti, ligi ya mataifa ya uefa hii hapa! Makundi na taarifa...

Usirudishe rimoti, ligi ya mataifa ya uefa hii hapa! Makundi na taarifa muhimu!

13486
0
SHARE

Kombe la dunia si limeisha? basi acha wafu wazike wafu wao. Wale waliodhani kwamba tunawarudishia rimoti tunawapa siku 53 tu Uefa hii hapa.

Ni alhamisi ya 6 Septemba Germany atapambana na France kwenye ufunguzi wa UEFA Nations League. Huku England v Spain kule Portugal v Italy.

Kwani UEFA Nations League ni kitu gani?

Hii ni michezo ya zile timu zenye uwezo sawa kukutana na kufanya ile michezo ya kirafiki kuwa ya kiushindani. Zile timu zenye alama nyingi zitawekwa kundi moja na kupigania nafasi ya kucheza fainali june mwaka 2019. Zile timu zenye uwezo mdogo zitawekwa makundi mengine ili kucheza kupigania nafasi ya kwenda juu. Katika kundi la timu zile bora timu itakayopata alama chache itashushwa daraja.

Mfumo:

Yatakuwepo makundi manne itakayojulikana kama ligi. Zitashiriki timu 55 baada ya Kosovo kuwa memba wa UEFA. Timu 12 zitaunda A, 12 Zitaunda ligi B, Timu 15 zitaunda ligi C, na 16 zitakamilisha ligi D. Kila kundi zitakuwa na makundi 3 au 4.

Kundi la timu zitakazopigania ubingwa huo

Ligi A
Pot Team alama No
1 Germany 40,747 1
Portugal 38,655 2
Belgium 38,123 3
Spain 37,311 4
2 France 36,617 5
England 36,231 6
Switzerland 34,986 7
Italy 34,426 8
3 Poland 32,982 9
Iceland 31,155 10
Croatia 31,139 11
Netherlands 29,866 12

Wale wa ligi A, watapambana kucheza fainali ya UEFA Nations League Finals. kutakuwepo na nafasi ya nusu fainali ya nyumbani na ugenini. Pia michezo yote ya kwenye makundi itakuwa na michezo ya nyumbani na ugenini.

Mgawanyiko wa ligi hii upoje?

Ligi A
Kundi 1 Kundi 2 Kundi 3 kundi 4
Netherlands Iceland Poland Croatia
France Switzerland Italy England
Germany Belgium Portugal Spain
Ligi B
Kundi 1 Kundi 2 Kundi 3 kundi 4
Czech Republic Turkey Northern Ireland Denmark
Ukraine Sweden Bosnia and Herzegovina Republic of Ireland
Slovakia Russia Austria Wales
Ligi C
Kundi 1 kundi 2 kundi 3 kundi 4
Israel Estonia Cyprus Lithuania
Albania Finland Bulgaria Montenegro
Scotland Greece Norway Serbia
Hungary Slovenia Romania
Ligi D
Kundi 1 Kundi 2 Kundi 3 Kundi 4
Andorra San Marino Kosovo Gibraltar
Kazakhstan Moldova Malta Liechtenstein
Latvia Luxembourg Faroe Islands Armenia
Georgia Belarus Azerbaijan Macedonia

Zile timu za makundi mengine matatu ya chini zitapata nafasi ya kwenda daraja la juu yaani ligi A kwa ajili ya mashindabo yajayo. Zinapanda timu 4 na kushuka 4.

Kwa mfano.

Ligi A itakuwa na makundi manne

Kundi 1
1. Ugiriki Alama 1000
Mikocheni Alama 100
Iraq alama 10

Kundi 2
Tanzania alama 20000
Chad alama 230
Msufini alama 3

Kundi 3
Rombo alama 4755
Bukoba alama 193
Sikonge alama 3

Kundi 4.
Mufindi alama 28374
Geita alama 1828
Sengerema alama 3

Timu zilizoshika mkia hapo zote zitakwenda Ligi B. Vivyo hivyo kwa timu za Ligi B zilizoongoza makundi yao zitapanda Ligi A. Na zilizoshia mkia ligi B zitakwenda ligi C, na C kwenda D

Tumeelewane hapo?

Droo ilifanyika kule Lausanne tarehe 24 Januari 2018. Timu zinazoshuka daraja ni zile za ligi A, B na C tu. Ligi D wataendelea kupambana na hali zao tu. Mashindano haya yatajirudia tena msimu wa 2020/21.

Wale washindi wa ligi A watapangiwa droo ya hatua ya mtoano Desemba 2018. Pia atakuwepo mshindi wa kwanza wapili watatu na wanne.

Mechi 1: 6–8 Septemba 2018
Mechi 2: 9–11 Septemba 2018
Mechi 3: 11–13 Octoba 2018
Mechi 4: 14–16 Octoba 2018
Mechi 5: 15–17 Novemba 2018
Mechi 6: 18–20 Novemba 2018
Droo ya Fainali: Desemba 2018
Fainali: 5–9 June 2019:

Fainali itachezwa kwa moja ya taifa ambalo limeandaa mashindano hayo. Fainali ni moja. Droo hiyo ya fainali itapangwa na uefa wenyewe

Je michuano ya kufuzu ya UEFA EURO 2020 itaingiliana vipi?

EURO itaendelea kawaida mpaka hapo itakapofika hatua ya mtoano. Kwa kawaida huwa fainali za Euro zinakwenda timu 24. Kwenye hatua ya makundi zinavuka timu mbili kila kundi (Jumla 20) na zitabakia nafasi nne. Timu hizo 20 ni zile zitakazoshika nafasi ya kwanza na ya pili katika makundi 10 ya kufuzu Euro. Hapo awali ilikuwa kuna hatua ya mtoano ili kuziba zile nafasi 4. Mwaka huu hatua ya mtoano hazitakuwepo tena ila zitapatikana kupitia Uefa national league.

Kivipi?
Kama nilivyosema awali kwamba kila ligi ina makundi yake. Kila mshindi wa kila kundi kwenye kila ligi atapata nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ili kufuzu Euro 2020 kama hakufuzu kupitia makundi ya kufuzu Euro.

Maelezo.

Kila ligi inatoa timu 4 ambazo hazijafuzu. Zitapatikana timu 16 ambazo zitacheza mtoano. Kisha zitatengwa kwenye makundi mapya ya kufuzu Euro.

Mfumo wa Makundi mapya ya mtoano ya Euro upo hivi:

Kila Ligi itapeleka timu 4 (Ambazo hazijafuzu kwa njia ya kawaida). Kama nilivyosema kila ligi ina makundi manne. Kila mshindi wa kundi ambaye hajafuzu kupitia hatua ya makundi ya Euro atapata nafasi ya kucheza hatua ya mtoano.
Kama kiongozi wa kundi la Uefa national tayari amefuzu kupitia Makundi ya Euro basi nafasi yake itachukuliwa na anayemfuata kwa alama.

Kwa mfano tuangazie na ligi A.

Ligi A ina makundi manne. Kila kundi litatoa timu moja inayoongoza kundi hilo ambayo haijafuzu.

Baada ya hapo kila timu za ligi A ambazo hazijafuzu ndizo zitaongoza makudi mapya ya mtoano.

Mfano wa Kundi
Ligi A: Timu 1
Ligi B: Timu 1
Ligi C: Timu 1
Ligi D: Timu 1

Makundi yapo manne hivyo utaratibu huo utafuata kwa makundi mengine matatu yaliyosalia.

Sheria zinainisha kwamba hakuna timu ya ligi moja itakutana na na timu ya ligi moja. Yaani timu za ligi A haziwezi kuwa kundi moja. Kila kundi litajumuisha timu angalau timu moja kutoka kila ligi.

Makundi hayo yatatoa mshindi mmoja ambaye atakwenda Euro.

Michezo ya Makundi Mapya itakuwaje

Timu ya ligi A Vs Timu ya ligi D
Timu ya ligi B Vs Timu ya ligi C.

Kisha washindi hukutana. Mshindi anakwenda Euro.

UEFA EURO 2020 Mtoano : 22 Novemba 2019. UEFA EURO 2020 Mtoano: 26–31 March 2020

Ikumbukwe Euro 2020 itafanyika kwenye miji 12 tofauti. Hakutakuwepo na nafasi ya moja kwa moja kwa muandaaji.

Waandaaji
Tarehe 12 June – 12 July 2020

Tuemelewana lakini?

Naitwa Privaldinho, usisahau kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here