Home Kimataifa Ukweli kuhusu kikundi cha “Pussy Riot” na kuvuruga fainali ya kombe la...

Ukweli kuhusu kikundi cha “Pussy Riot” na kuvuruga fainali ya kombe la dunia

22025
0
SHARE

Jana fainali za kombe la dunia zilipigwa, bao la kujifunga la Mario Mandzukic, lingine la Paul Pogba, Antoine Griezman na lile la Kylian Mbappe yakwapa ubingwa wa dunia timu ya taifa ya Ufaransa.

Kwa wale ambao hatukwenda Urusi kama bwana Shaffih Dauda tulishuhudia mchezo huu pale Escape One, katika mechi ile kuna tukio lilikuea likiendelea japo wengi tuliona kama linakatwa katwa na kujiuliza ni nini hiki.

Kulikuwa na kikundi cha mashabiki ambao kwa muonekano wa kawaida unaweza ukadhania ni scout ama ni askari lakini walikuwa wakiingia uwanjani na kutolewa kwa nguvu na maafisa usalama waliokuwepo uwanjani.

Moja kati ya picha iliyosambaa sana mtandaoni ni picha inayomuonesha mlinzi wa Liverpool Dejan Lovren akionekana kumkamata kijana mmoja kama anataka kumpiga, picha ambayo kila mtu alikuwa na maoni yake.

Wengi walimuona Lovren hana utu haswa kutokana na kijana huyo kuonekana akimpa mkono Mbappe na Mbappe akakubali, lakini kwanza kijana aliyekunjwa na Lovren na aliyempa Mbappe ni waawili tofauti, kuhusu Lovren alikuwa ana hasira, tuachane na hayo ni kwa nini haswa vijana wale walikuwa wakiingia uwanjani?

PUSSY RIOT. Ni nini hiki? Hili ni kundi la vijana ambao umri wao unatajwa kuanzia miaka 20-33 ambalo liliundwa mnamo mwaka 2011 na nia yao haswa ni kupingana na sera za raisi wa Urusi Vladmir Puttin wanayemuona kama gaidi, wamekuwa wanampinga haswa kwa kutumia sanaa na makongamano mtaani.

Inadaiwa kwamba kikundi hiki tangu wakati Urusi wakitangazwa kwamba watakuwa wenyeji wa kombe la dunia, wenyewe walijipanga kutumia fainali ya kombe la dunia kupeleka ujumbe wao kwa Puttin na serikali yake, bila kujali mechi ya fainali atacheza nani.

Walichoamua kufanya ni kuingia uwanjani ili iipe attention dunia kufahamu hawa ni wakina nani na kupitia jambo hilo dunia itafahamu ujumbe wao, na jana wakafanya hivyo mara nne wakaingia uwanjani.

Baada ya tukio hilo kutokea kikundi hicho kimetuma ujumbe sasa kuonesha nini wanakitaka na nini sababu haswa ya wao kuingia uwanjani na kufanya tukio kama lile katika mechi kubwa kama ile.

Kwanza wanataka wafungwa wote wa kisias walioko gerezani waachiliwe, hasa Oleg Senstov ambaye ni mtengeneza filamu wa kutoka Ufaransa ambaye amekamatwa nchini Urusi tangu mwaka 2014 kutokana na kupinga siasa za Putin.

Lakini  pili serikali ya Urusi iache kamata kamata inayoendelea ya watu wanaojihusisha na siasa nchini humo, tatu kuacha kufunga jela watu kwa mapenzi na chuki lakini nne wanasisitiza kuwepo na ushindani wa kisiasa nchini humo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here