Home Kimataifa Takwimu muhimu za yaliyojiri Urusi msimu mzima wa kombe la dunia

Takwimu muhimu za yaliyojiri Urusi msimu mzima wa kombe la dunia

9991
0
SHARE

Ufaransa tayari ni mabingwa na wamechukua kombe kibabe baada ya kuichakaza timu ya taifa ya Croatia kwa jumla ya mabao 4-2, lakini ukiachana na Ufaransa kuna rekodi mbali mbali za kufahamu kuhusu kombe la dunia.

Magoli na Pasi. Kumefungwa jumla ya mabao 169 katika msimu huu wa kombe la dunia, mabao haya yanatokana na shot on target 506 huku jumla ya mashuti 1623 yanepigwa na katika mashuti haya kumepigwa jumla ya pasi 59,255.

Timu kinara wa mabao haya ni Ubelgiji wakiwa na mabao 16, timu ambayo imefungwa sana msimu huu ni Panama ambao wamefungwa mabao 11, timu iliyomiliki sana mpira ni Hispania 71% na timu ambayo haikuwa ikikaa na mpira ni Iran 26.5%.

Epl kwenye kombe la dunia. Pamoja na kwamba Man City wanashikilia rekodi ya kuwa na wachezaji wengi kombe la dunia(15), lakini Tottenham inaongoza kwa wachezaji wao kucheza dakika nyingi katika michuano hii (5202).

Na Man City wenyewe wakicheza kwa dakika 4918, Manchester United waliokuwa na wawakilishi 11 walifanikiwa kucheza kwa dakika 4249 wakifuatiwa na Chelsea waliocheza kwa dakika 4231.

Cristiano Ronaldo. Kwa ujumla katika kombe la dunia ndiye mchezaji ana rekodi ya kukimbia umbali mrefu kwa muda mfupi km 21.1h, akifuatiwa na Ante Rebic wa Croatia km 21.0h na kisha Luis Advincula wa Peru 21.0h.

Bado tena Cristiano huyu huyu kwa sasa yeye ndiye anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa kuwahi kufunga hattrick, aliifunga siku ya mechi na Hispania akiwa na miaka 33 na siku 130, anafuatiwa na Rob Rensenbrink wa Uholanzi aliyewahi kufunga hattrick mwaka 1978 akiwa na miaka 30.

Sergio Ramos. Hawakushinda kitu lakini mlinzi wa timu ya taifa ya Hispania pamoja na klabu ya Real Madrid Sergio Ramos ndiye mchezaji aliyekamilisha pasi nyingi katika michuabo hii ya kombe la dunia 94.5%.

Dakika za majeruhi. Kama hufahamu tu ni kwamba hili ndilo kombe la dunia ambalo kuna mabao mengi ya ushindi yaliyofungwa dakika za lala salama, katika michuano hii kuna mabao 9 ambayo yalifungwa dakika ya 90+.

Suluhu ya 0-0. Hili ndilo kombe la dunia ambalo kumekuwa na idadi chache ya matokeo ya bila kufungana, na hiyo ilitokea mara moja tu wakati wa mchezo kati ya timu ya taifa Ufaransa dhidi ya Dernmark.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here