Home World Cup RUS 2018: Tukiachana na Mbappe na Modric, pia yupo Shaffih Dauda!

RUS 2018: Tukiachana na Mbappe na Modric, pia yupo Shaffih Dauda!

13044
1
SHARE

Kombe la dunia limeisha. Kilele cha yote kimetuletea majina mawili ambayo yatatawala vichwa vya habari. Huku Mbappe kule Modric. Wamefanya makubwa na wanahitaji pongezi nyingi. Kwetu sisi lipo la kujivunia zaidi. Nalo ni uwakilishi wa Shaffih Dauda.

Shaffih Dauda Kajuna ni mzaliwa wa Bukoba Kagera. Hivi sasa yupo Urusi. Anakaribia kurudi. Hakuenda kunywa wiski. Hapana. Ameenda kuangalia kombe la dunia lakini nyuma yake alikuwa na mambo yake mengine.

Kuna jamaa ameniuliza hivi Dauda ni mmasai?

Hapana! Dauda sio mmasai. Ukiangalia ile video unaweza kujiuliza mhhhh huyu Dauda vipi!!!!!!!!

Nikutoe shaka, Dauda ni mtu mzima na mwenye utimamu wake. Unaweza ukadhani labda kuna filamu anaigiza! Hapana! Sio muigizaji ila ni mdau wa soka tu.

Dauda naweza kumuita kama mshabiki aliyepata ushawishi mkubwa zaidi katika kombe la dunia la mwaka 2018! Cha kushangaza shabiki huyu ni Mtazania sio hata Mfaransa! Na timu ya taifa ya Tanzania haipo kombe la dunia. Wala hatuna mpango huo. Jambo la kujivunia ni kumuona Dauda yupo na bendera ya Tanzania.

Huenda wazungu wakaanza kumshangaa huyu jamaa kulikoni? Huenda wengine wakanza kugugo hiyo Tanzania nini? Mbaya zaidi hawawezi kukuta taarifa zozote za kiingereza kuhusiana na kombe la dunia na Tanzania.

Tulimuona Dauda amevaa rubega. Tena anaruka katikati ya Barabara hata jua halijazama. Angefanya hilo jambo pale taifa nadhani wangesema anatafuta kiki, zimemruka au hajielewi. Tungemtusi na kumnanga. Lakini kuna uwezekano wazungu pia wamemshangaa. Kila mzungu ana lake. Yupo atakayemdharau, yupo mzungu mbaguzi na yupo atakayepata burudani kwa kumuona kituko, pia yupo atakayeisoma akili ya Dauda.

Mnajua fika Warusi ni wabaguzi, Sio warusi tu kwanza niseme Wazungu wote ni wabaguzi. Ila tuliona Dauda akihojiwa na kituo cha Runinga cha Urusi. Wale Warusi kuna kitu wameona kwa Dauda. Huenda wanataka kuijua Tanzania vizuri. Tena Dauda akaokota kikundi cha Wazungu akaanza kuwaimbisha. Kama hilo halitoshi akawashika masikio Wabelgiji wakaanza kumuita Lukaku. Tena tulimuona akibadilishana fulana ya timu ya taifa ya Tanzania na Mbelgiji!

Hili nalo halitugusi!Au bado mnabishania VAR?

Kati ya Wazungu waliomuona kituko Dauda na Dauda mwenyewe nani amelamba dume?

Kwangu mimi Dauda! Kwanini? Kwa sababu amewajazia memori zao wakimrekodi. Siku wakirudi London, Paris au Brussels wataanza kuziangalia hizo picha na video. Na watatamani kuja Tanzania kuona hao Wamasai wanaishije na wapoje. Tena wakipata taarifa kuna mlima hapo watashawishika zaidi.

Bado huamini kama Dauda amewashika wazungu masikio.?

Uzuri ni kwamba alibeba bendera ya Tanzania. Wewe unadhani wandishi wa habari hawajamrekodi? Ni vile tu hamna team Dauda lakini tukipekenyua sana tungejua mengi.

Waandishi wangapi wamewaza haya! Unadhani Dauda amewaachia picha gani wale wazungu? Hivi angekuwa msanii wamuziki wa bongo fleva amefanya vile zile team zao za mitandaoni si mngemshinikiza Waziri wa Utalii akampokee Uwanja wa ndege siku akirudi?

Tumekuwa tukiamini kwamba wasanii wakifanikiwa kimataifa basi wanatangaza utamaduni wetu. Huu ni wakati muafaka kwa wasanii kuvalia njuga suala hili la kuitangaza Tanzania mara wakifika huko. Hasa hasa wakiwa stejini.

Hebu tujiulize Dauda ametumwa na nani? Nani aliyemwambia avae rubega? Je analipwa na wizara utalii? Je Dauda sio mtanzania? Je taifa star ipo Urusi? Tumeishia tumshangaa Shaffih lakini ni ngumu kumuona mdau wa soka akiweka picha au video ya dauda akimpongeza. Tutaishia kuwapost akina Mbappe na Modric lakini wametusaidia nini? Hata whawatujui. Huenda Modric hajui Tanzania ni nini? Je tutafanya makosa kumpa nafasi kubwa zaidi Shaffih! Ni wachache sana!

Wale tunaowapenda na kusema kwamba ni wachambuzi safi basi nao waige hili. Dauda ameenda sehemu ambayo asilimia 90 ya waliokwenda eneo hilo wamekwenda kwa ajili ya burudani. Dauda kaacha wiski kaanza kuruka ruka mchana kweupe. tunadhani kwamba alishindwa kwenda Zenji na familia yake? Je serikali imeona hilo?

Dauda anajua umuhimu wa jina lake na ubunifu atakaofanya utakuwa na tija kwa taifa. Achana na wale waonakwenda ulaya na kurekodi video za wanawake wapo nusu utupu kisha mnasema wanawakilisha taifa. Utaifa upi huo?

Dauda ametoa somo nini maana ya Uzalendo unapokuwa nje ya mipaka ya nchi yako. Sisi Tanzania tunawaona wamasai kama kabila la chini kustaarabika labda kwa kuwa wanaishi maisha duni lakini kumbuka Dauda ametumia changamoto hiyo kama chambo ya kuwanasa wazungu. Wapo viongozi wapenda sifa ambao wanapenda kudandia migongo ya wasanii waliofanikiwa. Natamani kuona hawa viongozi watamzungumzia vipi Dauda!

Dauda anapaswa kupewa tuzo ya heshima. Amefanya tukio ambalo ni wachache sana wapo tayari kufanya. Nimemkumbuka Bush alipokuja Tanzania. Kabila pekee alilolitambua ni Wamasai. Asante Dauda. Ni wachache watakuelewa. Wanasubiri tu uje umuongelee Manara kisha waje wamwage povu waseme hujui kuchambua mpira kama hao wasiopenda kuwaeleza ukweli.

Comments

comments

1 COMMENT

  1. Many times nimekua nikimpinga Shaffih Dauda katika mambo ya mpira hasa anapojipambanua yeye ni shabiki wa timu gani hapa Bongo… But for this.. Pongezi zangu zimfikie popote alipoo… Amefanya kitu cha msingi sana. Hongera broo Dauda Shaffih.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here