Home Kimataifa Ronaldo alivyokibadili kibibi kizee, sasa mambo saaafi

Ronaldo alivyokibadili kibibi kizee, sasa mambo saaafi

13369
0
SHARE

Watu walikuwa wanasubiri vipimo tu na hatimaye hii leo klabu ya soka ya Juventus imekamilisha vipimo vya mwanasoka Cristiano Ronaldo tayari kuwatukimikia.

Ronaldo amepewa jezi namba 7 kama kawaida ambayo alikuwa akiitunia Curdado na mwenyewe amekubali kuiachia jezi hiyo kwa heshima ya nyota huyo wa Ureno.

Tangu Juventus na Real Madrid kukubaliana kuhusu uhamisho wa Cristiano Ronaldo mambo yamebadilika kwa kibibi kizee cha Turin(Juventus) kuanzia mitandaoni hadi thamani ya klabu.

Unaambiwa siku sita tu baada ya Juve kutangaza kumpata Ronaldo thamani ya klabu hiyo katika soko la hisa imepanda kwa asilimia zaidi ya 20 tofauti na ilipokuwa mwanzo.

Huko katika social media ambapo ndio uwanja wa nyumbani wa Ronaldo mambo yamebadilika sana kuanzia Twitter, Face Book mpaka Instagram kuna mabadiliko katika kipindi kifupi sana.

Katika mtandao wa kijamii wa Instagram klabu ya Juventus imepata followers wapya zaidi ya milioni 1.5 katika siku hizi chache, Twitter nako Juventus wana followers wapya milioni 1.7 huku facebook wakiongezeka zaidi ya laki 7.

Madrid wakasirika. Ramon Calderon ambaye ni raisi mstaafu wa Real Madrid ametoa hisia zake kuhusu Ronaldo kutimkia Juventus akisisitiza kwamba hii ni mistake kubwa ambayo amewahi ona Madrid wakifanya.

Calderon alikuwepo Madrid wakati wakimnunua toka Manchester United 2009 na anasema kwa tabu waliyopata kumshawishi Ronaldo aliamini kwa uwezo wake wangemuacha acheze Madrid hadi achoke.

Amesisitiza kwamba duniani hakuna kama Ronaldo na hata auzwe kwa £100m au £1b sii lolote kwani ubora wa Ronaldo ni zaidi ya kitu chohote kile duniani 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here