Home Kimataifa Himid ameanza mazoezi Misri, kuna mengine usiyoyajua

Himid ameanza mazoezi Misri, kuna mengine usiyoyajua

9334
0
SHARE

Himid Mao ‘Ninja’ kwa sasa anajifua na timu yake mpya ya Petrojet huko Misri kujiandaa na msimu mpya wa ligi na mashindano mbalimbali.

Ninja ndio kwanza kajiunga na timu mpya kwenye nchi nyingine na ligi mpya, kuna vitu vingi vya kufahamu kuhusu maisha yake mpya akiwa Misri.

Leo kuna mambo manne ya kufahamu kuhusu Himid tangu aanze kufanya mazoezi na kikosi cha Petrojet,  amepokelewaje, nafasi yake kwenye timu, majukumu  aliyopewa na benchi la ufundi na vitu alivyojifunza hadi sasa.

Mwenyewe anasema amepokelewa vizuri kwenye timu na anapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu.

“Wamenipokea vizuri sana namshukuru Mungu napata ushirikiano wa kutosha hapa”- Himid Mao Mkami.

Unapoingia kwenye timu mpya unakumbana na changamoto ya kupambana kuonesha uwezo ili kulivutia benchi la ufundi kuhakikisha unapata nafasi ya kucheza, Himid analitambua vyema jambo hili.

“Nafasi ni ya kugombania kila siku katika maisha yangu, hiyo ndiyo nafasi yangu ya soka na sitobadili hilo.”

Alivyokuwa anacheza Azam na Taifa Stars mara nyingi alikuwa anacheza kama kiungo mkabaji wakati mwingine kama mlinzi wa pembeni lakini klabu yake ya sasa inampa uhuru zaidi kutokana na mfumo wa timu.

“Kila timu na kila mwalimu ana tofauti ya ufundishaji, hapa ni sehemu nyingine utamaduni mwingine najitahidi kuingia katika aina yao ya uchezaji, hapa napewa uhuru zaidi kwenye kucheza kwakua tunacheza viungo watatu.”

Ni muda mfupi ambao amekaa Misri lakini anasema kuna vitu vya kiufundi ameshajifunza ndani na nje ya uwanja.

“Mpira daima unaongeza kitu haijalishi unacheza nje au nyumbani, mechi au mazoezi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here