Home World Cup RUS 2018: Les Français sont champions du monde/ Ufaransa watwaa ubingwa wa...

RUS 2018: Les Français sont champions du monde/ Ufaransa watwaa ubingwa wa dunia

8163
0
SHARE

Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Ni safari ya mwezi mmoja ndani ya Urusi. Mabibi na Mabwana namleta kwenu mshindi wetu wa kombe la dunia 2018 UFARANSA!

Michezo 64 magoli 169 (2.59 kwa mechi. Asilimia 43% ni magoli yaliyopatikana kwa mipira ya kutengwa (adhabu na kona) kati ya magoli 169 ikiwa ni mabao 73. Hii ni idadai kubwa zaidi yokea mwaka 1966.

Mahudhurio yalikuwa 3,033,757 (46,885 kwa kila mechi)Mfungaji bora ni Harry Kane (6 magoli)

Hizi ni fainali ya 21 tokea michuano hiyo. Hii ni michuano ya mara ya kwanza kufanyika ulaya mashariki na ni michuano ya 11 kufanyika ulaya.

Jambo la kuvutia zaidi katika michuano hii ni VAR. Wapo walioipokea na wapo walioiktalia mbali.

Croatia wamepoteza mchezo huu fainali ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika hatua hiyo. Hii ni fainali ya 3 kwa ufaransa wakishinda moja mwaka 1998 na kupofeza ule wa mwaka 2006.

Mchezo wa leo mabao yamefungwa na

(Mandzukic 69)

(Mbappe 65)

(Pogba 59)

(Griezmann 38pen)

(Mandzukic 18 kujifunga.

Mambo yalikuwa hivi

⏰ 18′ – France 1-0 Croatia
⏰ 28′ – France 1-1 Croatia
⏰ 38′ – France 2-1 Croatia
⏰ 59′ – France 3-1 Croatia
⏰ 65′ – France 4-1 Croatia
⏰ 69′ – France 4-2 Croatia

Mchezo ulianza kwa kasi na kila timu ilionesha uwezo wake. Ufaransa wamefanikiwa kutwaa ubingwa huu kwa kucheza kwa kujihami zaidi. Oliver Giroud anabeba ubingwa huu akiwa kama mshambuliaji tegemezi ambaye hajafanikiwa kupiga shuti lolote lililolenga langoni.

Luka Modric na Ng’olo Kante wamepambana sana dimba la kati lakini Deschamps akaamua kumtoa Kante kwa hofu ya kulimwa kadi nyekundu. Modric ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa kombe la dunia. Kwa mara ya sita mchezaji bora wa dunia anatokea timu ambayo haijabeba ubingwa , (Messi, Forlan, Zidane, Khan na De lima).

Kylian Mbappe anawekza rekodi ya kuwa kijana wa pili tokea Pele mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao katika fainali hiyo.

Mlinda mlango wa Ubelgiji Thibaut ametwaa tuzo ya mlinda lango bora zaidi katika fainali hizi. Hii ni kwa mara ya kwanza kwa taifa hilo kutoa mchezaji bora katika kombe la dunia.

Takwimu za Bingwa
Mechi: 7
Wins: 6
Sare: 1
Magoli ya kufunga: 14
Magoli ya kufungwa: 5

Didier Deschamps anakuwa mwanadamu wa 3 duniani kuwahi kubeba komne la dunia kama mchezaji na pia akiwa kaama kocha. Wengine ni Mario Zagallo n Franz Beckenbauer.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here