Home Kitaifa Mkurugenzi Singida UTD amefunguka usajili wa Kaseke Yanga

Mkurugenzi Singida UTD amefunguka usajili wa Kaseke Yanga

11577
0
SHARE

Kuelekea msimu mpya wa kimashindano, suala la usajili linazidi kushika kasi, Yanga imemtambulisha Mrisho Ngasa na Deus Kaseke ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kucheza katika klabu hiyo.

Kaseke alijiunga na Singida United msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili lakini kabla ya mkataba wake na Singida haujamalizika amerudi tena Yanga swali linalojadiliwa ni je, Kaseke na Singida wamemalizana au yametokea mambo kama ya Fei Toto?

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema Singida United na Yanga vilikaa na kukubaliana kuhusu usajili wa Deus Kaseke na hawana tatizo katika usajili huo.

“Ni kweli Singida United ilikuwa na mkataba wa miaka miwili na Deus Kaseke na alikuwa ametumikia mkataba kwa mwaka mmoja lakini kulikuwa na makubaliano kati ya Yanga na Singida United kwamba mchezaji huyo atakwenda kuitumikia Yanga”-Festo Sanga.

“Kwenye hili hatuna tatizo, tatizo letu na Yanga ni kuhusu Fei Toto hilo ndio tatizo kubwa. Kuhusu Kaseke tupo sawa hatuna tatizo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here