Home Kimataifa “Ubelgiji ilistahili kucheza fainali kombe la dunia 2018 kuliko Ufaransa”-Shaffih Dauda

“Ubelgiji ilistahili kucheza fainali kombe la dunia 2018 kuliko Ufaransa”-Shaffih Dauda

8917
1
SHARE

Jana Ubelgiji walifanikiwa kuwa washindi wa tatu wa fainali za kombe la dunia 2018 baada ya kuifunga England kwa magoli 2-0.

Ubelgiji imetoa meseji kwa dunia kwamba ilijiandaa kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu ukiangalia namna walivyocheza na kiwango walichoonesha katika mechi zote kuanzia hatua ya makundi.

Huku na huko Shaffih Dauda huyu hapa, yeye kwa upande wake anasema Ubelgiji hawakustahili kucheza mechi ya mshindi wa tatu, yeye anasema walistahili kucheza fainali na kuwa mabingwa au washindi wa pili.

“Ubelgiji ni kikosi ambacho sio kimekuja tu Urusi kushiriki kombe la dunia ni timu ambayo imeandaliwa (project). Wakati wanaanza kuunganishwa pamoja ilikuwa ni mpango wa taifa la Ubelgiji pamoja na chama cha soka wakiwa wameweka mpango wa muda mrefu ili kufanya vizuri kwenye mashindano.

“Walianza kutengeneza academies ili kuzalisha vipaji vingi kama akina De Bruyne, Courtois, Kompany, Naigollani na wengine ambao wote ni kizazi kimoja.

“Ubelgiji ilikuwa inatarajiwa kufanya vizuri na kila mtu ameona ni timu ambayo haikustahili hata kumaliza katika nafasi ya tatu kwa mtazamo wangu. Ni timu ambayo ilistahili kucheza fainali, kwa upande wangu naona Ubelgiji walistahili kucheza fainali kuliko Ufaransa kutokana na project yao ilivyokwenda na timu yao inavyocheza.

“Wameonesha kiwango cha juu na matokeo waliyokuwa wakipata walistahili. Kwangu Ubelgiji ni moja kati ya timu bora ambazo zimenifurahisha kwenye mashindano ya mwaka huu (2018).

“Watu wengi wanaweza kusema walistahili kumaliza katika nafasi ya tatu lakini mimi siwezi kusema wamestahili kuwa washindi wa tatu, walistahili kushika nafasi mbili za juu kuwa mabingwa au nafasi ya pili kwa maana ya kucheza mechi ya fainali.

Jambo la kujifunza

Watu wengi walitarajia kuona mabadiliko makubwa kwenye vikosi vyote katika mechi hii ya mshindi wa tatu, waliamini wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye mechi zilizopita ndio ingekuwa mechi yao lakini ilikuwa tofauti kabisa.

Makocha wote waliitolea macho mechi hiyo, kwa kuonesha umuhimu wake walipanga wachezaji wengi waliocheza kikosi cha kwanza mechi zilizopita hata mabadiliko yaliyokuwepo likuwa ya kiufundi hayakuwa ilimradi tu mchezaji fulani nae acheze mechi ya kombe la duni.

“Level ya professionalism kwa wenzetu ipo juu sana, kuna baadhi ya watu mechi ya mshindi wa watatu wanaichukulia poa. Hii ni mechi ambayo ipo kwenye utaratibu kama mechi nyingine zote, mshindi wa tatu anapata sifa na ‘insentives’.

“Pia Fifa wana sisitiza kuupa heshima mchezo wa mpira wa miguu na wenzetu ambao wameendelea katika level za juu wanaelewa hilo.

“Hakuna mechi ambayo ya kuchukulia poa, hivi karibuni tuliona mechi ya EPL Stoke City wakiwa tayari wameshuka daraja walicheza mechi yao ya mwisho kwa nguvu zote kutafuta ushindi hii ndio inaonesha level ya professionalism hivi ni vitu vya kujifunza sisi ambao tunakua.”

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here