Home Kimataifa Takwimu muhimu kuelekea mchezo wa mshindi wa tatu Ubelgiji vs Uingereza

Takwimu muhimu kuelekea mchezo wa mshindi wa tatu Ubelgiji vs Uingereza

7078
0
SHARE

Ubelgiji waliondolewa na timu ya taifa Ufaransa katika mchezo wa nusu fainali huku Uingereza wakiondolewa na Croatia na hii leo timu hizo mbili zinapata nafasi kucheza mechi yao ya mshindi wa tatu.

Timu hizi zinajua kama unakumbuka Uingereza na Ubelgiji walipangwa katika kundi moja la michuano hii ya kombe la dunia ambapo timu ya taifa Ubelgiji waliibuka kidedea cha bao 1-0.

Hii ni mara ya pili kwa timu za taifa kukutana mara mbili katika msimu mmoja wa kombe la dunia, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2002 ambapo timu ya taifa ya Brazil na Uturuki nao walikutana mara mbili.

Ubelgiji pia hii sio mara yao ya kwanza kucheza katika hatua hii ya kumtafuta mshindi wa tatu, mwaka 1986 walicheza hatua hii dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa ambapo walifungwa mabao 4-2 katika extra time.

Mara ya mwisho kwa timu ya taifa ya Uingereza kushinda mechi nne  ilikuwa mwaka 1966 katika kombe la dunia na endapo leo watashinda watakuwa wameifikia rekodi yao ya 1966.

Endapo Harry Kane atafunga bao katika mechi ya hii leo baasi atakuwa mchezaji wa kwanza wa Uingereza kuwahi kufunga mabao zaidi ya sita katika msimu mmoja wa fainali za kombe la dunia.

Kama ilivyo kwa Ubelgiji, timu ya taifa ya Uingereza nayo imewahi kucheza mara moja mchezo wa mshindi wa tatu na ilikuwa mwaka 1990 walipocheza dhidi ya Italia na kupoteza kwa mabao 2-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here