Home Makala RUS 2018: Mgawanyo mzima wa fedha kombe la dunia! Bingwa anapewa kiasi...

RUS 2018: Mgawanyo mzima wa fedha kombe la dunia! Bingwa anapewa kiasi gani!

9883
0
SHARE

Ubelgiji na England wamegombania £18 milioni. Mchezo wa leo binafsi umeboa wengi. Wengi wamesema bora kuangalia katuni. Ulikuwa mchezo wa walioshindwa. Ile hari ya upambanaji hakuna. nimewonea huruma wale waliokwenda St Petersburg. Ni kama walikuwa msibani tu.

Gareth Southgate na vijana wake walikuwa na ndoto ya kubeba ubingwa wa dunia. Swali linakuja kwa changamoto ipi kubwa walookumbana nayo? Kucheza dhdi ya Panama na Sweden? Hapana!

Tuachane na hayo.

Fifa walitenga kiasi cha £302million kwa ajili ya maandalizi ya zawadi za kombe la dunia, mnamo October 2017.

Timu zote 32 zilipewa £1.2million kwa kufika fainali hizo.

Bingwa kati ya Ufaransa na Croatia ataondoka na Euro milion 30. Mshindi wa pili atajibebea Euro milioni 21.

Bingwa atapewa £29million pamoja na hela ya kuingilia £1.2m.

Ushindi wa Belgium siku ya leo umempa nafasi ya kujitwalia £18million kwa kumaliza nafasi ya 3, huku England akijizolea £16.5million.

Mgawanyo mwingine

Timu zilizotolewa nafasi ya robo fainali ziliondoka na kitita cha £12.1million. Timu zilizotolewa mafasi ya 16 bora zilijizolea kitita cha £9million.

Zile timu 16 Poland, Germany na Egypt ambazo zilizolambishwa mchanga kwenye hatua ya makundi zilijizolea kitita cha £6million.

Nafasi kiasi Jumla
Makundi $8m $128m
16 bora $12m $96m
Robo fainali $16m $64m
No 4 $22m $22m
No 3 $24m $24m
Msh. 2 $28m $28mMA
MABINGWA $38m $38m
TOTAL $400

Zawadi kwa mwaka 2014

Position Prize (per team) Total prize fund
Group Stage $8m $128m
Last 16 $9m $72m
Quarter-finals $14m $56m
Fourth place $20m $20m
Third place $22m $22m
Runners-up $25m $25m
Winners $35m $35m
TOTAL $358m

Kumbukumbu zinginezo

Mwaka 2002 mshindi wa tatu alitwaliwa Uturuki.

Mwaka 2006 mshindi wa tatu alitwaliwa ujerumani.

Mwaka 2010 mshindi wa tatu alitwaliwa Ujerumani.

Mwaka 2014, mshindi wa tatu alitwaliwa Uholanzi.

Mwaka 2018, mshindi wa tatu alitwaliwa Belgium.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here