Home World Cup RUS 2018: Uchambuzi kuelekea mechi ya fainali ya Ufaransa Vs Croatia

RUS 2018: Uchambuzi kuelekea mechi ya fainali ya Ufaransa Vs Croatia

9928
0
SHARE

Kuna mtu anaitwa Mark Ogden. Ametoa mtazamo wake kuhusu mshindi wa kombe la dunia.

Kule MOSCOW ndani ya Luzhniki Stadium kombe la dunia linafikia ukingoni.

Odgen amemsifia sana Didier Deschamps. Anamwamini nahodha huyu wa zamani wa ufaransa iliyotwaa ubingwa mwaka1998.

Mpinzani wa France ni Croatia.

Croatia wamefika fainali hizi kwa kuwaondosha Denmark, Russia na England (Tena wote ndani ya muda wa nyongeza) Pongezi kubwa kwa nyota wa Real Madrid mtaalamu Luka Modric ambaye wanamwamini kuwa atapeleka ubingwa huu kule kanda ya Balkans kwa mara ya kwanza.

Uchambuzi wake upoje?

Magolikipa!

France wanamtegemea Hugo Lloris ambaye alichomoa mkwaju wa Martin Caceres kwemye robo fainali vs. Uruguay, na ule wa Toby Alderweireld vs Belgium.
Lloris sio mzuri sana akiwa na mpira mguuni hivyo Croatia watajaribu kutumia udhaifu huu.

Danijel Subasic atabaki kuwa shujaa wa kuimbwa kwa taifa lake. Licha ya kupata majeraha kwenye mchezo wao dhidi ya Russia mlinda mlango huyu wa Monaco bado alisimama kidete kuhakikisha Waingereza hawamsumbui. Ogden haamini kama Subasic kukoa mikwaju miwili ya penati pekee inatosha, kwani Lloris ana uzoefu mkubwa wa mashindano makubwa.

Ulinzi

Timu zote France na Croatia zimeifungwa mabao 6. Croatia hawajawahi kutoka bila kuruhusu bao katika mchezo wowote wa hatua za mtoano.

Dhidi ya England, walinzi wake walisumbuliwa sana na Raheem Sterling, Jesse Lingard na Dele Alli, mabeki wao Dejan Lovren na Domagoj Vida walifanya kazi ya ziada.

France, pumzi yao ipo kwenye mapafu ya Kylian Mbappe, na safu yao ya ulinzi chini ya Samuel Umtiti na Raphael Varane ipo Imara.

Viungo
Croatia wa viungo walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana katika fainali hizi wakiongozwa na Luka Modric, Ivan Rakitic na Marcelo Brozovic, lakini watakutana na visiki vya N’Golo Kante, Paul Pogba na Blaise Matuidi. Kwenye vita ya dimba la kati Ogden anaamini kuwa wote wamelingana ubavu.

Washambuliaji.

France wamebarikiwa kuwa na kizazi chenye kila aina ya mshambuliaji kwa sasa kuliko timu yoyote kule Urusi.

Mbappe na Antoine Griezmann hawakamitiki. Mpira wa mabavu na juhudi wa Olivier Giroud umeipa France balansi nzuri na amekuwa kama egemeo imarakwa wachezaji wanzake. Deschamps bado ana uwanja mpana kwani benchi yupo Ousmane Dembele, Nabil Fekir na Florian Thauvin.

Croatia wao wanamtegemea veteran wao Mario Mandzukic akisaidiwa na Ivan Perisic pamoja Ante Rebic wanaotokea pembeni. Odgen anaamini kuwa wachezaji wa Croatia sio wazuri sana ila inategemeana na ufanisi wao. Mechi yao na Urusi walicheza hovyo lakini mechi na England walicheza vyema. Hivyo hawana kiwango cha kueleweka wanabadilikabadilika tofauti na Ufaransa.

Makocha
Deschamps alikuwa nahodha 1998 wakati wanabeba kombe la dunia, pia Champions League mara mbili, akiwa na Marseille na Juventus.

Zlatko Dalic alikuwa mchezaji wa kwaida sana ambaye hata hakuwahi kuwa mchezaji tegemezi kwa taifa lake. Alipewa nafasi ya kuionoa Croatia mwezi Octoba mwaka jana. Miaka ya nyuma aliwahi kufundisha Albania, Saudi Arabia na United Arab Emirates.

Dalic anaonekana wazi kuwa ameiacha timu ya Croatia kucheza kwa jitihada zao wenyewe. Tumeona mara kadhaa akiwapa nafasi kubwa na sauti uwanjani wachezaji wao tegemezi Modric, Rakitic na Mandzukic kufanya maamuzi.

Walipofika Croatia wamezidi hata matarajio na mipango yao. Haoni kama watajitoa sana hasa ukilinganisha hapo wamefika kwa ngekewa. Upande wa Deschamps, walipoteza fainali kwa Portugal kule Paris Euro 2016. Hivyo Deschamps yeye atacheza kwa umakini zaidi.

Odgen yeye ametabiri
France 3-1 Croatia

Hayo ni maneno ya Odgen sio yangu. Je wewe una mtazamo upi?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here