Home Kimataifa Hatimaye Djokovic ammaliza Nadal na kufuzu kwa fainali za Wimbledon 18

Hatimaye Djokovic ammaliza Nadal na kufuzu kwa fainali za Wimbledon 18

7443
0
SHARE

Hatimaye ule mchezo wa nusu fainali kati ya Rafael Nadal na Novacl Djokovic umepigwa tena hii leo na kama ulivyoisha jana Djokovic amampiga tena Rafael Nadal.

Masaa 5 na dakika 16 yalitosha kwa Djokovic kummaliza Nadal kwa ushindi wa seti 6-4, 3-6, 7-6,3-6,10-8 na sasa Djokovic anakuwa amebakiza mchezo mmoja tu kushinda Grand Slam yake ya kwanza tangu 2016.

Mchezo wa leo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mamilioni ya mashabiki kwani wawili hawa pamoja na kukutana mara 52 lakini hawajawahi kukutana katika mchezo mkubwa tangu fainali ya France Open 2014.

Hii inaweza kuendelea kuwa comeback nzuri kwa Djokovic kwani baada ya kutawala ulimwengu kwa muda alianza kupotea mwaka 2016 kutokana na majeruhi ambayo yalipelekea hadi akatoka kwenye 20 bora ya viwango vya tennis.

Kwa matokeo ya hii leo sasa Djokovic atakutana na Kevin Anderson raia wa Afrika Kusini katika mchezo ambao ndio utakaoamua bingwa wa michuano ya Wimbledon kwa mwaka 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here