Home Kimataifa Kylian Mbappe na mfupa uliomshinda Cristiano Ronaldo

Kylian Mbappe na mfupa uliomshinda Cristiano Ronaldo

14951
0
SHARE

Miaka 13 iliyopita katika jiji la Paris kama ilivyo kwa vijana wengi wenye ndoto ya kuwa kama mtu flani, Kylian Mbappe alikuwa chumbani kwake akizitazama picha za Cr7 na kutamani/kuamini siku moja atakuja kuwa kama yeye.

Kupitia mahojiano kadhaa ambayo Mbappe amefanya amekiri kwamba Cr7 ni kama kioo kwake na ndiye mtu anamuangalia kuweza kufika katika kilele cha mafanikio na anapambana kufika alipo.

Siku zinakwenda na majira yanasonga, miaka 13 baadae toka Mbappe apige picha hizo anakwenda katika fainali za kombe la dunia huku role model wake akiwa nyumbani na mpenzi wake Georginia wakiangalia mechi hizo kwenye luninga.

Kylian Mbappe anakwenda kucheza fainali yake ya kwanza kombe la dunia mfupa ambao Cr7 ameshindwa kabisa kuula, Kylian Mbappe anakwenda kufanya kile role model wake ambacho ameshindwa katika career yake yote.

Sii hivyo tu bali Kylian anakwenda katika fainali hii dhidi ya Croatia huku akiwa ametoka kuipita rekodi ya Cr7 ya mchezaji mwenye speed katika mashindano haya, katika mechi vs Argentina kinda huyu wa Kifaransa alikimbia kwa 38km/h.

38km/saa? Ndio, ndio Kylian Mbappe alikimbia kwa muda huo na kwa taarifa tu ni kwamba mkimbiaji nguli Usain Bolt anakimbia 44.72km/h na hapo unaweza kupata kuona namna speed ya Mbappe ilivyo kubwa.

Kama hufahamu tu ni kwamba Ronaldo ndiye amemjenga Mbappe, baba mzazi wa Kylian amesema wakati mwanae alipokuwa kijana mdogo alikuwa akitizama video za Ronaldo kwenye internet.

Katika umri wa miaka 19 na siku 192 Mbappe tayari ameingia katika vitabu vya rekodi za kombe la dunia akiwa ni kinda wa nne kuwahi kufunga katika michuano hii baada ya Pele, Michael Owen pamoja na Julian Green.

Ukiacha hilo lakini tayari Mbappe ameshavunja rekodi ya Pele anayetajwa kuwa mchezaji bora kuwahi kutokea dunia, na sasa Mbappe ndiye mchezaji mdogo kuwahi kufunga mabao mawili katika mechi moja kwenye kombe la dunia.

Ludovic Batelli ambaye ni kocha wa Ufaransa U-19 amewahi kufanya kazi na Cr7 pamoja na Mbappe na anakiri kwamba hawa wawili wote ni washindi na wana uwezo mkubwa lakini anaamini Mbappe ni bora zaidi kuliko Cr7 alivyokuwa na umri kama huu.

Mwaka 1998 wakati Ufaransa wanachukua kombe la dunia Thiery Henry, Lilian Thuram, Emmanuel Petit na David Trezeguet ni wachezaji ambao waliibeba Ufaransa na wote hawa wanne walikuwa wanatokea katika academy ya Fc Monaco.

Mwaka huu tena academy hiyo hiyo inamtoa Mbappe ambaye ndio nguzo katika mafanikio ya Ufaransa hadi sasa huku Vadim Vasilyev makamu wa raisi wa Monaco akisema hashtushwi na anachofanya Mbappe.

Vasilyev anasema tofauti na nyota wengine vijana katila soka, Mbappe yeye ni mtu wa kazi tu, “hawazi kotu kingine chochote katika maisha yake, anawaza soka na hata mapigo ya moyo wale yanadunda kwa ajili ya soka”. Huyo ndio Kylian Mbappe tunasubiria kuona kama atabeba kombe hili ambalo tayari Messi na Cr7 wanaonekana wamekwama kulibeba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here