Home Uncategorized Dechamps atoa sababu itakayowafanya Waafrika kuiunga mkono Ufaransa

Dechamps atoa sababu itakayowafanya Waafrika kuiunga mkono Ufaransa

12429
0
SHARE

Jumapili hii hapa baada ya miaka minne tunashuhudia mchezo wa fainali ya kombe la dunia na hapa ndio tutapata bingwa mpya atakayechukua nafasi ya Ujerumani ambao walitolewa tangu katika hatua ya makundi ya kombe la dunia.

Ufaransa vs Croatia, kila mtu ana sababu za kuchagua upande apendao katika fainali hii, lakini asilimia kubwa ya watu weusi wako upande wa timu ya taifa ya Ufaransa kwa sababu timu hiyo imejengwa na wachezaji wengi weusi na wenye asili ya Afrika.

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Dechamps amezungumzia uwepo wa Waafrika wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa na kukiri kwamba anatambua uwepo wa wachezaji wengi wenye asili ya Afrika katika timu yake na hili linawafanya wajivunie.

“Pamoja na kwamba sisi ni raia wa Ufaransa lakini natambua vijana wetu wengi asili yao ni Afrika na kule wana ndugu, jamaa pamoja na marafiki na hili linatupa moyo na kujivunia kuwakilisha watu wengi kutoka huko katika michuano hii” alisema Dechamps.

Paul Pogba, Kylian Mbappe, Samuel Umtiti, Matuidi na Ngolo Kante ni moja kati ya nyota ambao wako katika kikosi cha kwanza cha timu ya Ufaransa ambao watakuwa katika fainali hii kuikabili timu ya taifa ya Croatia.

Msimu huu ndio kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982 ambapo hakuna timu yoyote kutoka Africa imepenya kutoka hatua ya makundi lakini uwepo wa Wafaransa ambao wachezaji 12/23 wa kikosi chao ni weusi inawapa Waafrika cha kuzungumzia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here