Home Kitaifa “Usajili wa mchezaji sio kama bidhaa sokoni”-Shaffih Dauda kuhusu Fei Toto

“Usajili wa mchezaji sio kama bidhaa sokoni”-Shaffih Dauda kuhusu Fei Toto

12305
0
SHARE

Usajili wa Fei Toto bado unaendelea kuchukua headlines kutokana na kutambulishwa na vilabu viwili tofauti (Singida United na Yanga).

Mambo kama haya yanatokea kwenye soka japo kwa wenzetu ni mara chache sana kuona mambo ya namna hii.

Tanzania kuna vitu ambavyo tunatakiwa kujifunza kwa wenzetu, tusiangalie vitu kwa jicho la taarifa au ushabiki pekee, bali vitu vinavyotokea kwa wenzetu waliopiga hatua kwenye michezo tuvilete kwetu na kuvifanyia kazi.

Tumejifunza nini huhusu uhamisho wa Ronaldo kutoka Madrid kwenda Juve?

Tulianza kusikia tetesi Cristiano Ronaldo anatakiwa na Juve na haikuwepo taarifa rasmi kwamba wanamsajili Ronald.

Baada ya tetesi ikaja taarifa kwamba Juve na Madrid wameongea juu ya Juve kutaka kumsajili Ronaldo, wamekubaliana na Madrid wakairuhusu Juve ikazungumze na mchezaji akikubali warudi tena kwa uongozi wa Madrid.

Juve wakazungumza na Ronaldo, akawapa mahitaji yake na masharti wakakubaliana. Juve wakarudi kwa Madrid kuripoti kwamba wameshakubaliana na mchezaji.

Madrid na Ronaldo wakamalizana na Madrid wakamruhusu Ronaldo kuondoka. Taarifa ya kwanza walitoa Madrid kumuaga Ronaldo na kushukuru kwa huduma aliyowapa.

Taarifa ya pili ikatoka kwa Ronaldo akiwaaga mashabiki na kuelezea namna alivyoishi Madrid. Taarifa ya mwisho ikatoka Juve ambao walitangaza rasmi kumsajili Ronaldo.

Kwa hiyo hapa utaona issue ya usajili wa mchezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine ni process hasa mchezaji anapokuwa na mkataba na klabu fulani.

Ishu ya Fei Toto kilichopo hapa katikati ni kwamba mchezaji ndio kila kitu kwenye mambo ya usajili.

Usajili wa mchezaji wa mpira wa miguu sio kama bidhaa za sokoni kwamba ukiwa na pesa unaongea na muuzaji mkikubaliana bei anakupa mzigo unaondoka.

Maana yake haiwezekani klabu na klabu zikakubaliana pasipo ridhaa ya mchezaji mwenyewe lakini pia mchezaji hawezi kuingia makubaliano na klabu nyingine wakati anamkataba na klabu nyingine.

Usajili wa Fei Toto una taswira mbili, Singida United na Fei Toto walikubaliana wakasainishana mkataba na wakamtambulisha. Badae Fei Toto na Yanga wakakubaliana na akatangazwa.

Fei Toto inabidi aseme mwenyewe amekubaliana na klabu gani baada ya klabu yake ya JKU na hiyo ambayo yeye anataka kwenda kucheza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here