RUS 2018: Raisi wa Ufaransa atoa ofa kwa Koscienly, Deschamps na hatma ya taifa lao

  8985
  0
  SHARE

  Siku/Muda : Jumapili 15 Julai (12:00 EST).
  Mahali: Luzhniki Stadium, Moscow
  Chaneli: Kama sio dstv potezea
  Hadharani: Tukutane Escape One, Mikocheni kwenye skrini kubwa.

  Raisi wa Ufaransa Mh Macron amewaalika Laurent Koscielny & Dimitri Payet kwenye fainali za kombe la dunia. Wachezaji hawa wote walitarajia kuitwa katika vikosi vyao vya timu ya taifa lakini majeraha nayo yalikuwa yana mipango nao.

  Raisi atakwenda na wachezaji hao kama wageni wake ili kupata nafasi ya kusheherekea ushindi huo.

  Kikosi France hakishangazi sana kuwa fainali. Wadau wengi wanasema wamecheza hovyo hasa ukilinganisha na ubota wao. Madee anasema kama ufaransa hawatabeba kombe hili wajilaumu wenyewe. Lakini Enock Bwigane anaema sio kirahisi namna hiyo, Croatia wanacheza kitimu kuliko timu yeyote.

  Ningekuwa msemaji wa FFF ya Ufaransa ningewashauri wadau wa soka kama vyombo vya habari kukaa kimya. Unakumbuka sakata la waingereza la “Its Coming home” kuna rafiki yangu anaishi Birmingham Uingereza anasema ule wimbo wao maalumu wa waingereza wa kombe la dunia ulishika nafasi ya kwanza kwenye chat za muziki huko Uingereza kwa kuchezwa sana. Akaniambia kila redio ukifungua ni its coming home.

  Uzuri wa wafaransa ni waoga sana na wenyewe ni kama hawajiamini sana. Wanakumbuka kilichowatokea katika fainali ya Ulaya mwaka 2016. Wanafahamu lolote laweza kutokea. Wanaheshimu kila mechi. Hawadharau timu ndio maana utashangaa wanacheza vibaya kwa sababu muda mwingi wao wamacheza kwa tahdhari ya kutokuruhusu bao.

  “Hakuna aliyetuamini, na hii imefanya tucheze kwa tahadhari kubwa” nukuu ya Paul Pogba.

  Wapo nyuma ya dakika 90 au 120 kufikia rekodi yao waliyoweka miaka 20 iliyopita chini ya utawala wa Zinedine Zidane.

  “Hii ni mechi muhimu kabisa kuwahi kutokea katika maisha ya kila mchezaji wa ufaransa,” Maneno ya Hugo Lloris

  Kuna tofauti gani ya 2018 na 2016?

  Kuna maneno Pogba aliposema baada ya kuwaondosha Belgium kwemye vyumba vya kubadilishia nguo.

  “Hatupaswi kufanya makosa ya miaka miwili iliyopita,”

  Kauli hii aliongea kwa jazba kubwa na kwa sauti kubwa kila mtu kwenye chumba alishtuka!

  Unajua alimaanisha nini? Hakuna kucheza kwa kudharau mtu. Ni kama anawatahadharisha wenzake kwamba hawachezi na mabua ila wanadamu wenzao. Kocha mkuu Didier Deschamps alibaki kumtazama Pogba.

  Si unajua Pogba anapenda sifa? Akatudia tena “Hatujamaliza shughuli bado, kuna mchezo mmoja mkononi, hakuna haja ya kufurahia, bado kwanza, tushinde kwanza ndipo tufurahie”

  Pogba na wachezaji wengine 8 wanajua haswa nini kilichotokea Paris miaka miwili iliyopita mbele ya Ureno ambayo haikuwa na Ronaldo ndani. Walitoka kumfumua Germany mabao 2-0 kwemye nusu fainali na bado walipoteza fainali hivyo hawapaswi kibweteka na ushindi wao dhidi ya ubelgiji.

  “Tumesemwa sana, hasa baada ya kufungwa fainali kizembe na Ureno tena kwenye ardhi yetu” Haya yalikuwa maneno ya Olivier Giroud.

  Hofu kubwa ya Deschamps ni matokeo ya mchezo huo. Atawaambia nini wafaransa kama na hii watapoteza? Nani atamsikiliza? Yaani ataanzaje kwanza? Huo muda wa kujieleza atautoa wapi?

  Deschamps amekwemda Urusi akijiamimi sana.

  Deschamps “Kila mara hapa ufaransa najiona nipo sehemu sahihi na sijawahi kukosea” Maneno haya ni kama anamjibu Erix Cantona ambaye amekuwa mpinzani wake mkubwa.

  Deschamps ananena haya kwa kiburi kwa sababu anajua kama atakamilisha hili basi atakuwa mtu wa tatu kwemye historia ya kombe la dunia kutwaa ubingwa huo akiwa kama mchezaji na pia kama kocha. Wengine waliowahi kufanya hivyo ni Mbrazil Mario Zagallo (1958, 1962 na 1970) na jemedari la kijerumani Franz Beckenbauer (1974 na 1990).

  Deschamps alikuwa nahodha mwaka 1998 miaka 20 iliyopita na kama atafanikiwa wakati huu basi atajipiga kifua chake kisawasawa.

  Kila mchezaji anamwamini mwalimu wake. Na inaonekana wazi watapambana kwa ajili ya taifa lao pamoja na heshima ya kocha wao
  “Anahitaji heshima ya kila namn,” alisema Lloris. Ameandaa timu kwa malengo. Anatumia uzoefu wake kumsoma kila mchezaji na tabia zake. Hapendi mchezaji ajione bora kuliko wengine. Yupo sahihi kwa sababu hakuna mchezaji mkubwa kuliko ufaransa.”

  Deschamps hakuaminika sana. Ni wazi kwamba hata media za Ufaransa zilimrushia sana mawe. Deschamps hapendi sana kubabaishwa. Na ni mtu ambaye haogopi kufanya maamuzi kwa sababu tu fulani hatopendezwa nayo. Deschamps ni tofauti kidogo na kocha wa Argentine ambaye alifanya kazi kuwaridhisha watu fulani.

  Kuna kitu Deschamps huwa anakiamini sana, “strong defence na legendary luck”. Ulinzi thabiti pamoja na kushinda kwa nafasi. Yaani haumizi kichwa namna ya kutengeneza mafasi ya mabao ila anaamini hayo mambo yapo tu uwanjani yanakuja yenyewe kikubwa ni kujilinda.

  “Timu inapaswa icheze ninavyotaka mimi na sio mchezaji anavyojisikia kucheza” Alisema

  Unakumbuka maneno ya Cantona kwa Deschaps? Alisema Didier ana jitihada kubwa, anaweza kucheza hadi jasho linaisha lakini hana kipaji. kwenye suala la kipaji yeye na mbeba maji hana tofauti. Ni kweli Didier huwa haangaliagi mchezaji ana hwezo gani ila anajituma kiasi gani. Hili lipo sawa ndio maana amewaacha watu kama Martial na Lacazette ambao wao wanachezaJi zaidi kwa sababu ya uwezo wao lakini hawajitumi sana uwanjani.

  Hili lipo wazi sana kwani Deschamps na wenzake walishinda kombe la dunia 1998 kutokana na uwezo wao mkubwa wakukaba na kujituma.

  Pogba ndiye mchezaji aliyekomaa zaidi kiakili na kiupambanaji kwenye hii timu. Amekuwa mstari wa mbele nje na ndani ya uwanja kuhamasisha wenzake. Hakika anastahiki pongezi.

  Sio Pogba tu, pia yupo mzaliwa wa 1993 Raphael Varane. Sababu kubwa ya Wabelgiji kurudi nyumbani anayo huyu mwanaume

  Varane ni kama Pogba, alikuwa na miaka 21 mwaka 2014, pale alipozidiwa ujanja na Mats Hummels, wakati ufaransa ikipoteza mchezo huo wa robo fainali. Miaka minne baadae anaruka kichwa mbele ya wachezaji wenye nguvu na warefu wa Uruguay na kuivusha Ufafansa kwa bao lake.

  Pia yupo bwana mdogo Kylian Mbappe. Ana miaka 19, hatuwezi kusema ni kiongozi bado lakini tumbwili lake utadhani ana miaka 25.

  1998 = 2018?
  Deschamps alikuwa mwanafunzi wa Aime Jacquet, mwaka 1998 mwaka huu yeye ndiye mwalimu huenda akatumia mbinu za mwalimu wake kutwaa ndoo.

  Kama Jacquet, Deschamps amewaacha wale wachezaji wanaotumia zaidi nyenzo ya vipaji kujitafutia nafasi kama Anthony Martial, Adrien Rabiot. Jacquet nae alifanya hivyo.

  France walitwaa ubingwa 1998 wakiwa na safu ya ulinzi hatari. Mabeki wake watatu walifunga mabao, Bixente Lizarazu, Laurent Blanc na Lilian Thuram. Mwaka huu mambo ni yale yale, Benjamin Pavard, Varane and Umtiti nao wameweka kambani mabao.

  Olivier Giroud amekuwa na michuano mibovu lakini bado hari yake na uchu wake wa upambanaji ni ule ule. Anafanya kazi katika mazingira magumu na bila shaka yupo chini ya kivuli cha mafanikio ya timu. 1998 ufaransa ilikuwa na mtu kama Grioud alijulikana kama Stephane Guivarc’h.

  Na Privaldinho (Instagram).

  Comments

  comments

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here