Home Uncategorized RUS 2018: Mambo 20 tuliyojifunza Kombe la dunia

RUS 2018: Mambo 20 tuliyojifunza Kombe la dunia

8023
0
SHARE

1. Maradona anapaswa kupumzika. Madawa sio Maziwa ya pakti. Umri umeenda. Ana Mengi ya kufanya kuliko kujidhalilisha

2. Senegal walikuwa na nguvu na udi. Lakini wametukumbusha kwamba, msuli tembo mafanikio kisoda. Walikuwa na uwezo lakini hawakucheza kitimu.

3. Kuna Ronaldo mmoja, kuna Messi mmoja na kuna Luka Modric mmoja tu

4. Mzimu wa mabingwa ulionekana kwenye chumba cha malaika Joachim Low. Low hakutaka kusikia ishauti wa yeyote alijiona yupo sawa katika maamuzi yake yote.

5. Argentine wana matatizo kama aliyo nayo Maradona. Hakuna dhuluma inayodumu.

6. Neymar alipaka sana poda mwisho wa siku kaishia kufanana na yale maajini ya bongo movie (Kituko)

7. Waingereza walikwenda kwenye sherehe kupitia mlango wa uwani hawakujua kama kwenda kula lazima uwe na tiketi.

8. Iran, Japan na Korea wametupita afrika mbali sana. Kuna uwezekano mchezaji wa Asia akabeba Ballon miaka 10 ijayo kuliko timu ya afrika kufuzu hatua ya Robo fainali.

9. Kombe la dunia lilikuwa na wachezaji wenye asili ya Afrika mashariki watatu (Pione Denmark-Mganda, Poulsen Denmark-Mtanzania, Olsson Sweden -Mkenya) Afrika mashariki tuna damu ya vipaji shida ni fursa tu.

10. VAR ni chombo cha uchunguzi lakini nadhani kinapaswa kianze kuchunguzwa chenyewe kwanza.

11. Uaminifu ni kila kitu. Mashabiki wa Japan walisafisha uwanja na wachezaji wao pia hawakuacha hata ganda moja la bablishi kwemye vyumba vyao.

12. Kombe la dunia la mwaka huu halikuwa la kubeti kabisa. Korea 2-0 German, Croatia 3-0 Argentine.

13. Kiatu cha mfungaji bora wa mwaka huu hakipaswi kuwa cha dhahabu. Ni chepesi mno. Labda apewe yeboyebo (Natania). Harry Kane Mabao 6 ( Penati 3, mabao mawili yaliparaza watu, limoja la kichwa).

14. 2002 Brazil walibeba kwa sababu walikuwa na vipaji, 2006 Italia walibeba kwa sababu walikuwa na wachezaji wazoefu, 2010 Hispania ilibeba kwa kucheza soka safi, 2014 Ujerumani walibeba kwa kupambana, mwaka huu hata malaika wenyewe nahisi hawaelewi kilichotokea, Vipaji Brazil nje, Jitihada Ujerumani chali, Hispania soka safi holaa, Hao Italia taarifa zao hatuna.

15. Urusi wametuonesha hata kama watu wanakudharua vipi, lakini familia yako ikiamua kukusapoti utafika mbali. Urusi kucheza nyumbani kumempeleka hadi hatua ya Robo fainali. Urusi hii hii ambayo haikushinda mchezo hata mmoja wa kirafiki kwa miezi 6 ikamkazia Hispania.

16. Ama kweli ng’ombe wa Masikini hazai. Yaani Senegal na nguvu zao zote lakini wametolewa eti kisa wana kadi za njano nyingi…!!!

17. Viongozi wa nchi wana hamasa kubwa katika soka.

18. Kukazwa kwa sheria za soka kumefanya nidhamu iongezeke kwa kiasi kikubwa. Hakuna vurugu kila timu inacheza soka safi.

19. Kombe la dunia sio kombe la nchi zinazomtegemea mchezaji mmoja.

20. Pigania taifa kwanza. Ustaa weka pembeni kuna wachezaji tumeona kiburi kimewarudisha nyumbani. Kwa mfano Kalinic amefukuzwa kambi ya Croatia baada ya kukataa kuingia uwanjani zikiwa zimesakia dakika 5. Kisha akafukuzwa wakati wa michuano ya makundi. Leo taifa lake lipo fainali yeye anazunguka tu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here