Home World Cup RUS 2018: kiburi na majivuno, yamekatisha ndoto ya kucheza fainali

RUS 2018: kiburi na majivuno, yamekatisha ndoto ya kucheza fainali

8009
0
SHARE

Uvumilivu ni silaha kubwa sana kwenye mafanikio ya kila mwanadamu. Subira ni akiba. Ukiwa na haraka sana unapoteza vingi. Unaweza ukajaliwa vingi lakini unaposhindwa kuwa mvumilivu na kukubaliana na mazingira basi unapoteza kila kitu.

Si mnamkumbuka Carlos Teves? Alikuja kama staa ila kwa sasa hakuna mwenye habari nae? Alikosa uvumilivu, hakuwa tayari kusikilia. Subira kwake ilikuwa mtihani.

“Croatia walikwenda kombe la dunia na washambuliaji asilia wawili tu. Mario Mandzukic, jamaa aliyewaliza Waingereza na Nikola Kalinic anayekula bata gizani kwa sasa. Ilikuwa ni riski kubwa sana kwa Croatia kwani hawakua na mshambuliaji mwingine mzuri zaid yao.

Tatizo linapokuja ujue linakuja na fursa.

Penda kutumia changamoto za maisha kama njia ya kufanya kitu kikubwa zaidi. Kalinic alishindwa kutumia nafasi ya majaribu aliyoyapata. Aliabudu hisia zake. Alijiona kama hakutendewa haki.

Nacer Chadli anapaswa kuwa fundisho la kwanza kwa Kalinic. Nacer alitokea benchi mchezo wao na Japan. Hakuna aliyejua kama hatma ya Ubelgiji ilikuwa benchi. Alitokea benchi na kuwarudisha Wajapan Tokyo kichwa chini miguu juu. Huenda angeanza asingewekwa kwenye historia hiyo.

Kosa la Kalinic ni lipi?

Croatia walicheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Nigeria. Kalinic alikuwa benchi akisiburi Mandzukic apumzike au yeyote. Lakini yeye aliamini kwamba yeye ni bora. Akili yake haikuwa sawa na alijawa na hasira. Zikiwa zimesalia dakika 5 mwalimu alimuita aingie uwanjani.

Kalinic kwa hasira aligoma kusimama. Akaishia kulalamika. Hakuona sababu ya yeye kuachwa benchi. Mawazo yake alidhani kwamba hakuna anayemzidi yeye ubora. Akamjia kocha juu akaonesha ghadhabu yake waziwazi.

Hakuona umuhimu wa zile dakika 5.

Kukaa benchi sio ugonjwa. Wala sio dhambi. Kalinic amesahau kwamba Ole Gunnar Solskjær aliwekwa benchi mechi ya fainali ya UEFA licha ya kuhusika kwenye mabao mawili kwenye mechi ya FA Cup Fainali. Ole Gunnar aliingia zikiwa zimesalia dakika 10 na akafanya maajabu. Kuwekwa benchi haimaanishi kwamba hujui. Wakati fulani unaambiwa ukiwa vitani usipende kutoka na silaha zako zote. Na waalimu huweka wachezaji muhimu benchi ili kuwaleta baadae kuongeza nguvu zaidi.

Kalinic aligoma kuingia ndani kisha nafasi ile kutwaliwa na Pjaca. Maakocha wasaidizi na viongozi walimjia juu Kalinic lakini hakuomba radhi.

Baadae mwalimu akamtimua. Kalinc kula bata na kuweka picha akiwa na watoto wazuri mitandaoni akila maisha. Kwenye akili yake hakudhani kama Croatia ingefika mbali. Alijua tu muda sio mrefu wataungana nae. Hata mimi sikiwahi kuwaza kama Croatia watafika mahali.

Aibu kubwa sana kwake. Timu imefanikiwa bila hata ya msaada wa kivuli chake. Huko aliko anajionaje? Ataishi vipi na watu mtaani? Au ndio atatengwa kama Barbosa alivyotengwa kule Brazil?

Timu ya taifa sio sehemu ya kuonesha ufalme. Wanajeshi 22 wamebaki Urusi mpaka fainali. Wachache mno wenye majina makubwa kwenye kundi hili lililokubali kupiga magoti kwa taifa lao. Kalinic anaonekana kama msaliti tu. Ataishia kuishi kwenye taifa lake kama mtumwa kisa tu amejiona mkubwa.

Hata wewe jifunze kuficha hisia zako mbele ya jamii. Maisha wakati fulani hayana usawa lakini usipende kujionesha kwamba wewe unafaa kuliko wengine. Kuna wakati maisha yanahitaji yaongee zaidi kisha wewe uyasikilize. Kalinic hapa bongo wapo wengi wala sitaki kuwataja majina.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here