Home Kimataifa Muafrika Kusini avunja rekodi Wimbledon iliyodumu kwa miaka 97

Muafrika Kusini avunja rekodi Wimbledon iliyodumu kwa miaka 97

7822
0
SHARE

Rekodi imeandikwa hii leo katika michuano inayoaendelea ya Wimbledon wakati wa mchezo kati ya Kevin Anderson raia wa Afrika Kusini na John Isner raia wa Marekani na hii leo ikiwa nusu fainali.

Anderson alifanikiwa kumbwaga mpinzani wake John Isner katika nusu fainali ambayo ilichukua muda wa masaa 6 na dakika 35 kwa ushindi wa seti 7-6, 6-7, 6-7, 6-4, 26-24 na hii inakuwa mechi ya pili kwa urefu katika historia ya tennis.

Kabla ya mchezo kati ya Kevin Anderson dhidi ya John Isner rekodi ya mchezo mrefu wa tennis ilikuwa ikishikiliwa na mchezo wa fainali ya SW19 mwaka 2013 kati ya Djokovick na Juan Del Potro mchezo uliopigwa kwa masaa 6 na dakika 43.

Mchezo unaoshikilia rekodi kuchezwa kwa muda mrefu zaidi ni mechi kati ya Leornardo Mayer raia wa Argentina na Joao Souza raia wa Brazil mchezo ambao ulipigwa kwa muda wa masaa sita na dakika 43.

Mara ya mwisho kwa mchezaji kutoka Afrika Kusini kucheza fainali ya Wimbledon ilikuwa mwaka 1921 Brian Norton alipokwenda fainali na sasa Anderson anaivunja rekodi hiyo iliyodumu kwa miaka 97.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here