Home Kitaifa Video-Miaka 20 ya George Kavila kwenye ligi anahitaji nini kama si heshima?

Video-Miaka 20 ya George Kavila kwenye ligi anahitaji nini kama si heshima?

8037
0
SHARE

Vuta picha mwaka 1998 ulikuwa na umri gani, ukikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini?

Tangu wakati huo ni miaka 20 sasa imepita, mambo mengi mazuri na mabaya yamepita kama mtoto alizaliwa mwaka huo kwa sasa ni kijana ambaye kwa mujibu wa sheria za Tanzania anaruhusiwa kuoa na kuolewa.

Mabibi na Mabwana namleta kwenu moja ya ma-legendary wa VPL George Kavila ambaye ameitumikia ligi ya Tanzania bara tangu 1998 (miaka 20 sasa). Kwa kifupi ameanza kucheza ligi kuu kabla ya Kabwili, Mkomola, Kibabage, na wengine wengi hawajazaliwa hadi leo bado anatwanga nao.

Katika miaka 20 aliyocheza ligi ya Tanzania amedumu Kagera Sugar kwa miaka 10 (ambako yupo hadi sasa) na miaka 10 mingine imegawanyika katika vilabu mbalimbali.

Kavila amekutana na mikasa mingi ambayo unatakiwa kuifahamu, kwakuwa mimi ni jukumu langu kukupa mikasa hiyo nimemtafuta Kavila na amesimulia kila kitu mwanzo mwisho.

Wachezaji wengi wa timu ambazo hazina majina makubwa wanaogopa kucheza mechi dhidi ya Simba na Yanga, Kavila anasema mechi hizo anazipenda sana anatamani kila siku acheze dhidi ya Simba au Yanga.

Wachezaji wana mengi ya kujifunza kutoka kwake kwa nini yupo kwenye game hadi leo tena kikosi cha kwanza halafu kwenye benchi wamekaa vijana kibao wanasubiri!!

Msimu ujao (2018/19) utakuwa wa mwisho kwake kucheza soka la ushindani, baada ya hapo atastaafu kuwapisha vijana.

Kavila amecheza kwa muda mrefu zadi ligi kuu Tanzania bara (kwa wachezaji wanaocheza hadi sasa) akifuatiwa na Shabani Nditi wa Mtibwa Sugar aliyeanza kucheza ligi kuu msimu wa 1999/2000.

Tumpe heshima anayostahili mtu huyu #GeorgeKavilaIsOurLegend

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here