Home Kimataifa Shaffih Dauda alivyochungulia uhamisho wa Ronaldo kwa jicho la biashara

Shaffih Dauda alivyochungulia uhamisho wa Ronaldo kwa jicho la biashara

13233
0
SHARE

Uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid kwenda Juventus ni uhamisho ambao unaangaliwa kwa angle ya 360, ukiuangalia kwa kawaida utakufanya uumie utashindwa kufikiria ni aina gani ya biashara imefanyika.

Ukifatilia kwa dunia ya sasa hivi ambayo mpira wa miguu umehamia pia nje ya uwanja, uhamisho huu wa Ronaldo unagusa sehemu nne ambazo mmoja utaathirika mwingine unapata faida lakini mwisho wa siku ilibidi uhamisho ufanyike ili upande ambao tunaona utapata hasara tuone kama hasara itatokea.

Uhamisho huu unamgusa mwenyewe mchezaji, unagusa klabu ya Real Madrid, unagusa klabu ya Juventus, na unagusa Seria A pamoja na La Liga kwa sababu uhamisho wa mchezaji una athari pia kwenye ligi.

Kama unakumbuka kipindi kile Neymar anakwenda ligi ya Ufaransa kulikuwa na vita kubwa sana kati ya bodi ya ligi ya La Liga ambao hawakuwa tayari kumshuhudia Neymar anaondoka kwenye ligi yao kwenda ligi nyingine matokeo yake anakwenda kuipa nguvu ligi nyingine na wao wanashindana wanataka La Liga ibaki juu iwe na biashara nzuri kutokana na kuwa na wachezaji wazuri.

Kwa hiyo Seria A kwa kumpata Ronaldo itapata boost, ukiangalia tangu miaka ile ya Ronaldo de Lima alipohamia Seria A ilikuwa na heshima lakini kwa miaka ya karibuni imeonekana kuwa ligi ya kawaida kwa hiyo inapopata mchezaji kama Ronaldo anakwenda kuiongezea thamani na kuipa attention kwa maana ya kufatiliwa na dunia nzima.

Kwa upande wa Juventus £100m na gharama zote ni zaidi ya £300m ukijumlisha ada ya uhamisho, mishahara na bonus, pesa hizi Juve wanazitoa wapi? Itazirudishaje hayo ndio majibu yanayosubiriwa kutoka kwa familia ya Agnelli kuona maamuzi yao yalikuwa yamelenga nini kama ni brand yao ya magari ya Fiat na Jeep au wanataka klabu yao kufatiliwa na ulimwengu mzima ili iwe rahisi kwao kufanya biashara katika level ya dunia.

Kuwa na mchezaji kama Ronaldo ambaye anatambulika kidunia ni faida kwao kwa sababu atawafanya watambulike kidunia na waweze kufatiliwa kwa ukaribu na makampuni makubwa hivyo watafanya biashara kwa muda ambao atakuwa kwao.

Wanaweza kumfanya balozi wa klabu akawa anashiriki katika events mbalimbali ambazo zinaihusu klabu na bidhaa zake kwa hiyo nafikiri wamemchukua Ronaldo kwa upande huo hawajawekeza kwake kwa ajili ya kushinda Seria A kwa sababu tayari wameshashinda mara saba mfululizo. Hawajamhitaji Ronaldo kwa ajili ya kufika fainali ya Champions League kwa sababu katika miaka minne iliyopita wamefika fainali mara mbili labda asaidie kuchukua ubingwa.

Kwa mtazamo wangu, uwekezaji wa Juventus kwa Cristiano Ronaldo ni kwa ajili ya kuwasaidia kuwapa thamani nje ya uwanja na si ndani ya uwanja. Kingine wameondokewa na wachezaji wakongwe kama golikipa wao Gigi Buffon Stephan Lichtsteiner, Kwadwo Asamoah imewasaidia kupata budget kumnunua Ronaldo huenda Higuani akaondoka. Licha ya wakongwe hao kuondoka bure, ukipunguza budget yao ya mishahara ukaongeza kiasi kingine unapata pesa ya kumnunua Ronaldo.

Ronaldo anaondoka La Liga kwenye klabu ambayo tayari ameshinda Ballon d’Or mara tano, ameshinda mataji manne ya Champions League (marabtatu mfululizo) ameshinda La Liga ni klabu ambayo inaheshimika kimataifa anapokwenda klabu kama Juve anaathirika? Kwa sababu anakwenda kwenye klabu ya chini kidogo, ambayo itamlazimu ang’ae ili thamani yake isishuke akiwa na umri wa miaka 33 hatutarajii kumuina kiwango chake kinashuka ukilinganisha na alivyokuwa Real Madrid.

Kwa hiyo na yeye ana changamoto, amepewa mkataba wa miaka minne anajua kwamba anatakiwa kufanya kazi ya ziada kuendelea kuwa bora katika miaka minne inayokuja. Anafahamu akishindwa kuonesha uwezo maana yake thamani yake itashuka na biashara zake zitashuka japo hataathirika moja kwa moja kiuchumi kwa sababu tayari ameshakuwa tajiri.

Real Madrid wao hawajapata hasara kwa sababu wamepata €100m wametengeneza faida ya £8m kwa sababu walimnunua £92m kutoka Manchester United. Uwekezaji walioufanya kwa Ronaldo tayari umeshalipa, amewapa mataji ya Champions League, La Liga, amekuwa mfungaji wa muda wote wa klabu amevuja rekodi mbalimbali za La Liga. Miaka tisa aliyokaa wamepata faida kubwa wamefanya biashara nje ya uwanja, thamani ya klabu imeongezeka.

Kumuuza £100m mchezaji mwenye umri wa miaka 33 na kukata budget ya mshahara wa karibia £55m kwa upande wao naona wamefanya biashara kubwa ambayo imekuwa na faida naamini ndio maana hata hawakutumia nguvu nyingi walipofutwa na watu wa Ronaldo kwa ajili ya kuhama.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here