Home Kimataifa Shaffih Dauda kataja sababu za Ubelgiji kupotea kwa wafaransa

Shaffih Dauda kataja sababu za Ubelgiji kupotea kwa wafaransa

9596
0
SHARE

Jana Jumanne July 10, 2018 ilichezwa nusu fainali ya kwanza ya kombe la dunia ambapo Ufaransa ilishinda 1-0 mbele ya Ubelgiji kwenye uwanja wa St. Petersburg.

Ukiachana na matokeo hayo, Shaffih Dauda ambaye alikuwa shuhuda wa mchezo huo ameulelezea mchezo huo ndani na nje ya uwanja.

Ndani ya uwanja amefanya uchambuzi akieleza sababu za Ubelgiji kupoteza mchezo huo licha ya kutabiriwa kufika fainali baada ya kuitoa Brazil katika mchezo wa robo fainali. Nje ya uwanja amezungumzia kuhusu mashabiki wa Brazil kuwa wengi kwenye mchezo huo na kuishangilia Ufaransa lakini pia issue ya tiketi.

Mabadiliko kwenye kikosi cha Ubelgiji

Kulikuwa na ingizo la Mousa Dembele na kubadilishwa position  kwa winga Nacer Chadli ambaye alikuwa anaziba pengo la Thomas Meunier ambaye alisimamishwa kwenye mchezo wa jana.

Mabadiliko ya kimfumo yalionekana kuigharimu Ubelgiji na ilicheza chini ya kiwango ukilinganisha na mechi zilizopita hadi wakafika hatua ya nusu fainali na watu wengi kuipa nafasi ya kufika fainali na kushinda ubingwa wa fainali za mwaka huu.

Kwa nini Ubelgiji ilicheza chini ya kiwango?

Tatizo kubwa ilikuwa ni mabadiliko ya kimfumo yaliyomfanya Dembele kuanza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza.

Kuanza kwake kukaifanya Ubelgiji kuwa na viungo wawili ambao walikuwa slow (Fellaini na Dembele), Witsel ni mkabaji kwa hiyo mipira ilikuwa haitembei haraka matokeo yake De Bruyne na Hazard walikuea wanachelewa kufikiwa na mipira hali iliyopelekea Lukaku kukosa huduma.

Mwisho wa siku muda unakwenda timu ikashindwa kucheza vizuri. Chadli katika nafasi ya beki wa kulia aliyocheza alikuwa anaonekana hatari wakati timu yao inamiliki mpira akawa anasogea juu kucheza katika nafasi yake ya asili lakini Ufaransa walipomiliki mpira ilimlazimu acheze kama beki kitu ambacho kilimgharimu na kuwampa nafasi kubwa sana Griezmann na Matuidi kutumia upande wake kuidhuru Ubelgiji.

Hadi mapumziko 0-0

Kipindi cha pili kona iliyopigwa kushoto ikamkuta Umtiti akapiga header kambani hadi dakika 90 mechi ikamalizika Ufaransa 1-0 Ubelgiji na Ufaransa wakaingia fainali ya kwanza tangu 2006 walipofungwa kwa matuta na Italia.

Uwanja wa St Petersburg ulikuwa na mashabiki wengi kutoka mataifa tofauti-tofauti lakini mashabki wengi wa Brazil waliendelea kuwepo uwanjani pamoja na timu yao kutolewa na Ubelgiji kwenye hatua ya robo fainali.

Mashabiki wengi wa Brazil walioingia uwanjani walikuwa wanaishangilia Ufaransa walikuwa na hasira na Ubelgiji kwa sababu iliifunga Brazil na kuitoa mashindanoni. Baada ya game kumalizika mashabiki walikuwa wanashangilia ushindi wa Ufaransa wakifurahia Ubelgiji kupoteza.

Kuna ambao waliondoka na jana walikuwa wanuza tiketi zao nje ya uwanja, huwezi amini tiketi ya category 1 ambayo thamani yake halisi ni $750 ilifika hatua ikawa inauzwa hadi $250 kwa maana ya pungufu kwa $500.

Tiketi zilikuwa ni nyingiambazo zilikuwa zinauzwa na ikasaidia watu wengi kuingia uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here