Home Kitaifa Mtibwa yachomoa Dilunga kwenda Simba

Mtibwa yachomoa Dilunga kwenda Simba

12098
0
SHARE

Mtibwa Sugar imepangua tetesi zinazomhusisha mchezaji bora wa kombe la TFF (FA Cup) 2018 Hassan Dilunga ambaye pia ni mchezaji bora wa Mtibwa Sugar kwa msimu uliopita kwamba huenda akajiunga na Simba.

Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Jamal Bayser amesema Dilunga bado ana mkataba na timu yao na wanaamini atamaliza mkataba wake.

“Taarifa za Dilunga kuhusishwa na Simba zinazungumzwa sana lakini suala la Dilunga kwenda Simba kwa sasa halipo. Hizo ni tetesi ambazo ni kawaida katika kipindi cha usajili”-Bayser.

“Dilunga bado ana mkataba wa mwaka mmoja na tunatumaini atamalizia mkataba wake ndani ya Mtibwa Sugar.”

Dilunga amewahi kucheza Yanga lakini baadaye akaondoka na kwenda kwenye vilabu ambavyo havina majina makubwa VPL lakini kwa sasa anafanya vizuri akiwa na Mtibwa Sugar.

Bayser amesema maandalizi kwa ajili ya msimu ujao yanaenda vizuri na tayari wamesajili mchezaji mmoja Jafar Kibaya ambaye alikuwa Mtibwa msimu wa 2016/17 msimu uliopita alicheza Kagera Sugar.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here