Home Kimataifa “Its not coming home”, Croatia waiondoa Uingereza kombe la dunia

“Its not coming home”, Croatia waiondoa Uingereza kombe la dunia

9921
0
SHARE

Dakika 5 tu zilitosha kwa Uingereza kuonesha nini walikuwa wakikitaka baada ya bao lililotokana na mpira wa adhabu ndogo lililofungwa na Kieran Trippier.

Tangu mwaka 1966 baada ya Portugal kufunga mabao 8 kwa mipira ya kutenga(set pieces), hakuna timu iliwazidi kwa mabao ya aina hiyo lakini bao la Kieran Trippier limewafanya England kufunga mabao 9 ya set pieces msimu huu wakivunja rekodi hiyo.

Wakati matumaini ya Waingereza yakiwa juu kuumaliza mchezo katika dakika 90, dakika ya 68 Ivan Perisic aliwanyanyua Croatia kwenye viti baada ya kufunga bao la kusawazisha.

Bao la Ivan Perisic ni la 4 kwake kwa msimu huu na ni Davor Suker tu ndiye amefunga mabao mengi kuliko Ivan Perisic kwa Croatia katika msimu mmoja wa kombe la dunia(mabao 4).

Dakika 90 za mchezo huo ziliisha kwa sare ya bao moja kwa moja ndipo muamuzi wa pambano hilo alipoamua kuongeza dakika 30 za mchezo huo.

Katika dakika 30 za nyongeza Mario Mandzukic dakika ya 109 alikatisha ndoto za Waingereza za kuupeleka ubingwa nyumbani baada ya kufunga bao la pili liloipeleka Croatia fainali ya michuano hiyo.

Kwa matokeo ya hii leo Croatia sasa atacheza fainali yao ya kwanza kombe la dunia dhidi ya Ufaransa, huku Uingereza wenyewe wakicheza na timu ya taifa Ubelgiji katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here