Home Kimataifa Watoto walionusurika kifo wakwama kwenda kombe la dunia, Pogba awazawadia

Watoto walionusurika kifo wakwama kwenda kombe la dunia, Pogba awazawadia

9860
0
SHARE

Siku hizi mbili uwanja wa habari za michezo umechangamka, nusu fainali ya kombe la dunia, huku Wimbledon, Ndondo Cup, Cristiano Ronaldo kwenda Juventus na huko Thailand kuna hii issue ya Wild Boars Fc.

Hawa ni timu ya soka ya wototo ambao walinusurika kifo baada ya pango ambalo walijabanza wakikwepa mvua kufunikwa na kifusi cha mchanga na kukaa humo kwa siku 17 lakini siku ya jana Jumanne walifanikiwa kuokolewa wakiwa salama.

Baada ya habari hii kutoka, shirikisho la soka ulimwenguni FIFA liliguswa na jambo hili na likaona ni bora wawape nafasi watoto hawa kusafiri hadi Urusi kushuhudia fainali za kombe la dunia.

Lakini taarifa za madaktari kutoka nchini Thailand zinasema hali ya kiafya ya watoto hawa bado haijakaa sawa na wanaweza kukaa kwa siku 6 hadi 8 hospitali na hii inafuta matumaini ya wao kwenda Moscow kwa fainali siku ya Jumapili.

FIFA wameeleza kwamba baada ya mualiko kwa watoto hao kukwama baasi watatafuta tukio jingine kubwa ambalo wanaweza kuwaalika vijana hao ambao almanusra ndoto zao za soka zizimwe.

Naye kiungo wa Manchester United mara baada tu ya timu yake ya taufa kufudhu kwa fainali ya kombe la dunia 2018 alikwenda Twitter kuandika ujumbe kuhusu ushindi wa Ufaransa na tukio la nchini Thailand.

“Ushindi wetu wa leo ni zawadi kwa watoto wa Thailand, safi sana vijana hakika muna nguvu”, Pogba na wenzake sasa wanasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili hii leo kati ya Uingereza na Croatia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here