Home Kimataifa Ufaransa yatangulia fainali kombe la dunia

Ufaransa yatangulia fainali kombe la dunia

6551
0
SHARE

Matumaini ya timu ya taifa ya Ubelgiji kwenda katika fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia yameshindikana baada ya kufungwa na Ubelgiji hii leo.

Kipindi cha kwanza katika mechi hii kiliisha kwa sare ya bila kufungana huku kukiwa na piga nikupige katika milango ya timu zote lakini hakuna timu iliyopata bao.

Kipindi cha pili dakika ya 51 timu ya taifa Ufaransa walipata kona, na Antoine Griezman ndiye alikwenda kupiga kona hiyo iliyozaa bao lililofungwa na mlinzi wa Barcelona Samuel Umtiti.

Bao la Umtiti linamfanya kuwa mchezaji mdogo kuwahi kufunga katika nusu fainali kombe la dunia(miaka 24 na miezi 7), rekodi ambayo imedumu miaka 60 tangu Just Fountaines kufunga mwaka 1958 akiwa na miaka 24 na miezi 10.

Hii ni ya kwanza tangu mwaka 1998 ambapo timu ya taifa ya Ufaransa inakuwa na mabeki watatu ambao wamefunga katika msimu mmoja wa kombe la dunia (Pavard, Varane na Umtiti).

Olivier Giroud alicheza kwa dakika 85 kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Steven Nzonzi, Giroud sasa anakuwa amecheza dakika 425(zaidi ya masaa 7) bila kupiga shuti kwenye lango la wapinzani.

Tangu 1998 baada ya timu ya taifa Ufaransa kufudhu kwa fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza hakuna timu ambayo imefika kombe la dunia mara nyingi kuwalita(3).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here