Home Kimataifa Trump aungana na Manchester United, Bayern Munich na As Roma kuhusu tukio...

Trump aungana na Manchester United, Bayern Munich na As Roma kuhusu tukio la Thailand

8227
0
SHARE

Hatimaye timu ya waokoaji nchini Thailand imefanikiwa kuwaokoa vijana 12 ambao wanadaiwa kufukiwa na kifusi cha mchanga siku chache zilizopita wakati walipokua katika mazoezi ya mpira.

Inadaiwa kwamba siku 17 zilizopita watoto hao pamoja na kocha wa timu yao walikuwa wakifanya mazoezi na wakati wamepumzika ikaanza kunyesha mvua iliyowalazimu kujibanza katika pango.

Wakati wamejibanza katika pango hilo kwa bahati mbaya mvua ile iliangusha kifusi cha mchanga ambao uliwaziba, hali iliyopelekea maisha yao kuwa hatarini.

Lakini hii leo kupitia ukrusa wa Face Book wa jeshi la waokoaji la Thailand waliandika “hatuna uhakika kwamba hii ni miujiza lakini watoto na kocha wao wote tumefanikiwa kuwatoa katika pango”

Baada ya ujumbe huo kusambaa dunia nzima, raisi wa Marekani Donald Trump hakusita kuficha hisia zake kutokana na tukio hilo na akatuma salamu kwa jeshi hilo la uokoaji kupitia akaunti yake ya Twitter.

“Kwa niaba ya wananchi wa Marekani, ninatoa pongezi kwa kikosi cha uokoaji cha Thailand kwa kuwakoa vijana wote 12 na kocha wao, ni nyakati nzuri sana, kazi nzuri” aliandika Trump.

Klabu ya Manchester United nayo haikubaki nyuma kuhusu suala hili la Wild Boars na kupitia mtandao wao wa Twitter wametoa ofa kwa vijana hawa kwenda Old Traford pamoja na kocha wao.

“Manchester United tunafahamu kilichotokea nchini Thailand na tungependa kuwakaribisha Wild Boars Fc na benchi lao la ufundi katika uwanja wa Old Traford kwa msimu wa ligi unaokuja”

Bayern Munich nao wamesema wamefarijika sana kusikia tukio la Thailand watoto walivyookolewa na wanawatakia kila la kheri katika soka lao la baadae.

As Roma wamesema hii ni habari kubwa zaidi katika soka kwa siku za hivi karibuni na kutuma pole kwa familia ya Suman Kunan aliyefariki wakati akiwa katika hatua za kuwaokoa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here