Home Kimataifa Taarifa rasmi ya Real Madrid kuhusu Cristiano Ronaldo

Taarifa rasmi ya Real Madrid kuhusu Cristiano Ronaldo

9967
0
SHARE

Hatimaye klabu ya Real Madrid imevunja ukimya kuhusu sakata la Cristiano Ronaldo na jioni hii wametoa taarifa rasmi kuhusu nyota huyo na inasomeka kama ifuatavyo.

“Real Madrid CF imekubaliana na maombi yaliyotolewa na mchezaji Cristiano Ronaldo aliyetaka kujiunga na klabu ya Juventus.

Leo, Real Madrid inataka kutoa shukrani kwa mchezaji huyu ambaye amethibitisha kuwa bora duniani na ambaye ameweka alama katika historia ya klabu yetu na soka la dunia.

Zaidi ya matajia aliliyoshinda, na mafanikio ayiyopata katika miaka hii 9 Cristiano Ronaldo amekuwa mfano wa kujitolea, kmpambanaji na mwenye kipaji kikubwa.

Pia amekuwa mchezaji bora katika historia ya Real Madrid na mabao 451 katika michezo 438. Katika  jumla ya 16, ikiwa ni pamoja vikombe vya Ulaya 4, 3 kati ya hivyo ikiwa mfululizo na 4 katika misimu 5 iliyopita.

Mafanikio binafsi akiwa na jersey ya Real Madrid ameshinda mipira ya 4 dhahabu, na kiatu cha dhahabu mara 3 ikiwa ni moja kati vingi alivyoshinda.

Kwa Real Madrid Cristiano Ronaldo daima atakuwa moja ya alama zake kubwa na kumbukumbu ya kipekee kwa kizazi kijacho.

Real Madrid daima itakuwa nyumba kwako daima.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here