Home World Cup RUS 2018: Taarifa kuelekea mchezo wa Ubelgiji Vs Ufaransa

RUS 2018: Taarifa kuelekea mchezo wa Ubelgiji Vs Ufaransa

7038
0
SHARE

Tunaangalia mechi ya leo Jumanne ya nusu Fainali, ya Kombe la Dunia kati ya France na Belgium, itakayochezwa uwanja wa Krestovsky muda wa saa 3:00 usiku.

Hizi ni taarifa za timu

France: Kiungo Blaise Matuidi amerudi, baada ya kusimamishwa mechi iliyopita kutokana na kupata kadi mbii za njano, na anaweza kwenda moja moja kwenye kikosi cha kwanza badala ya Tolliso, ambaye aliziba nafasi wakati wa mechi ya robo Fainali dhidi ya Uruguay. Didier Deschamps ataendelea kuwa na imani na Olivier Giroud kwenye eneo la mbele, japokuwa mshambuliaji huyo wa Chelsea, bado hajafunga goli au kupiga hata shuti lililolenga goli mpaka sasa. Kylian Mbappe amekosa mazoezi Jumatatu, wakati N’golo Kante na Benjamini Pavard walifanya mazoezi, wakiwa mbali na kundi la wachezaji muhimu, wakati Deschamps akijaribu kuweka timu timu yake sawa kwaajili ya mechi, lakini anatarajia kuwa na kikosi chote kilichokamilika.

Belgium: Wanakutana na wakati mgumu, na beki wao wa kulia Thomas Meunier amesimamishwa. Hivyo inamaanisha kwamba Nacer Chadri na Yannick Carrasco, wataanza kama mabeki wa kupandisha team kurudi kukaba, Vinginevyo Roberto Martinez anakutana na mvurugo kwenye safu ya ulinzi. Imebaki kuona kama Martinez ataendelea na Kelvin Debruyne kwenye eneo la kuanzisha mashabulizi au atamuita tena Dries Martens.

Je, unajua kwamba

Pande zote mbili zimekutana mara tatu katika mashindano makubwa, France akishinda mechi zote tatu walizokutana.

Belgium hawajafungwa katika mechi zao tatu zilizopita za kirafiki, walizokutana na France, wakishinda mechi moja na kutoa sare, mechi mbili.

Hii itakuwa nusu fainali ya sita, ya France ya Kombe la Dunia, France wamepoteza mechi tatu, za kwanza( 1958, 1982, 1986), lakini wameshinda mechi zilizopita, 1998 na 2006.

Ukiondoa matuta, France wamepoteza mechi moja ya mashindano yaliyopita ya Kombe la Dunia katika mechi za mtoano, wakishinda mechi 10, Sare 2 na kupoteza mechi 1.

Hii itakuwa mechi ya pili ya Belgium ya nusu Fainali ya Kombe la Dunia.

Belgium hawajafumgwa mechi zao zote 24, (wameshinda 19, Sare 5, kupoteza 0)

Vikosi vinavyoweza kuanza

France: Lloris, Pavard, Varane, Umtiti, Hernandez, Pogba, Kante, Mbappe, Griezmann, Matuidi, Giroud

Belgium; Coutois, Alderweired, Kompany, Vertongen, Carrasco, Fellain, Witsel, Chadri, Hazard, Lukaku, De Bruyne.

Habari na Aziz Mtambo

Mawazo yangu Privaldinho
Ni mchezo mgumu sana na nina imani upande huu ndio utakaotoa bingwa wa mashindano haya.

Dhamira yangu inanituma kwamba huenda mwaka fainali ikazikutanisha timu ambazo hazijawahi kubeba ubingwa huu fainali au timu ambayo haijawahi kubeba kabisa kubeba.

Ufaransa ina wacheza wazuri mno. Ina wachezaji wenye uwezo binafsi lakini wanafeli katika kuunganisha mawazo yao kuwa na lengo moja. Kuna mdau nimemwambia hilo akaona kama nina wivu nikamwambia kama Mchezo wa Ufaransa na Argentine Mbappe angecheza chini ya kiwango basi tungeongea mengine.

Wabelgiji wanacheza kama nyuki yaani wote kwa pamoja wamafuata mahali mpira uliopo. Wanajirundika sehemu moja wote ili kuweka presha. Faida yao kubwa ni kuwa na wachezaji wazuri mno kuanzia dimba la kati kwenda juu.

Shida ya Ufaransa ni kwenye sehemu ya ubunifu. Wanamtegemea zaidi Pogba na Tolliso. Hakuna aliyemwepesi ispokuwa faida ya Pogba ni mipira mirefu. Benchi yupo Matuidi mwenye pumzi licha ya kwamba nae anaonekana amechoka.

Ubelgiji wameshinda mechi zao 10 za mwisho za kombe la dunia. Shida nayoiona kwao hasa safu ya ulinzi ni mabeki wake. Hakuna beki ambaye ana wastani wa alama zaidi ya 6 kutokana na viwango vya whoscored.com. Wakati huo huo upande wa pili nao wameonesha uzembe mkubwa wa kuruhusu mabao matatu dhidi ya Argentine. Mchezo wao dhidi ya Uruguay kila mmoja aliongelea kukosekana kwa Cavani.

Safu ya Ushambuliaji ya Ubelgiji ni hatari sana. katika michezo yao 8 kati ya 9 ya mwisho wamefunga mabao zaidi ya mawili. Katika michezo 10 hawajafunga mabao chini ya mawili

Upande wa Ufaransa wao wamefunga mabao 6 kati ya 7. Kwa asilimia 99.8 Deschamp amefeli kumuamini Giroud mbele ya Laccazete. Giroud ameshindwa kupiga shuti hata moja au kufunga bao lolote licha ya kutoa pasi moja ya goli pekee.

Mchezo utakuwa na mabao mengi sana endapo tu timu moja itafanikiwa kupata bao kipindi cha kwanza. Licha ya kwamba nikiwaangalia vizuri Ubelgiji wao wana uwezo mkubwa sana wa kuzuia.

Dembele anahitajika sana ila kupooza mashambulizi na kucheza mpira wa kiume na akina Kante.

kwa mawazo yangu naona kama Ubelgiji anaweza kusonga mbele kwa sababu ina wachezaji hatari zaidi Hazard na De bruyne.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here