Home World Cup RUS 2018: Hawa Croatia watapata tabu sana kuwazuia England

RUS 2018: Hawa Croatia watapata tabu sana kuwazuia England

11456
0
SHARE

Jason Burt, mwandishi wa kujitegemea wa The Guardian ameweka karata yake kwa Raheem Sterling kuwa atawasumbua zaidi Croatia.

Ni kweli, kumekuwa na muunganiko mzuri wa Sterling na Harry Kane, licha ya kwamba Sterling amekuwa akilaumiwa sana na baadhi ya mashabiki kuwa amekuwa na mambo lukuki uwanjani.

Nina wazo tofauti hapa. Safu ya Ulinzi ya Dejan Lovren na Domagoj Vida ni wepesi na wana nguvu sana. Kipi ambacho Sterling anachoweza kuwaziddi hawa watu?

Upande wa pili ni kwamba, Kane ana uwezo mkubwa wa kupambana na hawa watu kwa nguvu lakini kwa Raheem mhhhh napata wasiwasi.

Sterling aliwasumbua sana safu ya ulinzi ya Sweden chini ya Andreas Granqvist na Victor Lindelof. Raheem amekuwa na kasumba ya kukosa nafasi muhimu za magoli licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuleta mashambulizi mengi kwa wakati muafaka.

Tukiachana na Raheem upande wa kocha mkuu Gareth Southgate, kwenye akili yake ana imani kubwa na Harry Kane ambaye amekuwa akimsumbua Lovren. Tottenham Hotspur walipokutana Liverpool Kane alimtesa sana Lovren ambaye alitolewa mara baada ya dakika 30.

Mfumo utakuwaje?

3-5-2

England hawajabadilisha mfumo tokea kombe la dunia lianze mpaka mchezo wa mwisho dhidi ya Sweden ambao walitumia mfumo wa 4-4-2.

Je una tija?

Bila shaka hakuna mtu asiyemjua Modric, pia walio wengi tunamfahamu vyema Rakitic. Ukiangalia uwezo walio nao hakuna kiungo wa kiingereza anayeweza kuthubutu kusimama nao kiufundi. Thsishangae kumuona Dele Alli akibeba jukumu la kukaba kama ilivyokuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Colombia. Kwenye mchezo wa Sweden tulimuona Alli akizurura tu licha ya kufunga bao. Southgate mwenyewe anakiri kwamba ameshindwa kupata matunda sahihi kwa Delle na anaamini mtihani wake wa mwisho ni mbele ya Modric. Kuna uwezekano mkubwa Fabian Delph au Eric Dier wakasimama nyuma ya Jordan Henderson ili kudhibiti makali ya Modric.

Mipira ya adhabu ni tatizo

Croatia wanapaswa kuwa makini sana na mipira iliyokufa. Kwa England wamefunga magoli 8 kati ya 11 kupitia mipira iliyokufa. Hii ni rekodi kubwa katika michuano ya kombe la dunia tokea Portugal walipofanya hivyo mwaka1966.

Sweden walishindwa kumzuia Harry Maguire kufunga bao kwa kichwa kupitia mpira uliokufa na hii inaonesha ni kwa namna gani England wapo makini sana na mipira ya juu. Croatia wanapaswa kuwa makini mno. Narudia mno

Maguirre na John Stones ni warefu na hiyo ndiyo faida kubwa. Kwa haraka haraka tu, Maguire 1.95m, Harry Kane 1.88m, John Stones 1.88m hata Alli ana 1.88m, hawa wote anayewakaribia urefu ni Lovren mwenye 1.88 ila Vida ana 1.84.

Tena mbaya zaidi ina wapiga krosi wazuri Kieran Trippier na Ashley Young.

Umakini wa washambuliaji wake

England wamefunga mabao 10 kati ya mashuti 13 yaliyolenga golini.

Geti laJordan Pickford

Wakati Gareth Southgate anamteua Pickford kuwa mlinda lango namba moja watu wengi walimjia juu na kudai kuwa hataweza kuibeba England mikononi mwake. Wapo walioamini kwamba Jack Butland alipaswa kuvaa glovs za taifa hilo lakini kitendo cha Pickford kuchomoa mikwaju ya penati nadhani wengi walifyata. Pickford amekuwa golikipa mdogo kabisa wa England kutokuruhusu lango lake kufungwa akiwa na umri wa miaka 24 na sikua 122.

Taarifa Muhimu

England dhidiya Croatia utachezwa pale Luzhniki Stadium, jijini Moscow, siku ya Jumatano saa 3 usiku.

Tomu hizi zote zimekutana mara 7. England wakishinda mara 4, Wakipoteza mara 2 na kutoka sare mchezo mmoja.

England na Croatia walitoka sare 0-0 mwaka 1996 kabla ya England kushinda 3-1 kwemye mchezo wa kirafiki mwaka 2003.

England walishinda ushindi wa 4-2 kwenhe michuano ya Euro mwaka 2004 Wayne Rooney akiizawadia England mabao mawili. l

Baadae Croatia wakaalipiza kisasi kwenye michuano ya Euro mwaka 2008 kwa kuwafumua England mabao2-0 kule Zagreb – kwenye rekodi zangu zinaeleza kwa Paul Robinson alofunga bao la kideo.

Mbaya zaidi ni pale Croatia walipowashika sharubu hawa wanajiita Simba wa tatu kwa kugawa kipigo cha mbwa koko pale pale Wembley Novemba mwaka 2007 kwa mabao 3-2 na kuwaondoa Emgland katika kinyang’amyiro cha kufuzu Euro 2008.

England walifanikiwa kushinda michezo yake miwili dhidi ya kwenye World Cup 2010 kwemye michezo ya kufuzu September 2008 (4-1) na September 2009 (5-1).

Wasiwasi wa Gareth Southgate ni Jamie Vardy, ambaye anasumbuliwa na Maumivu.

Croatia kwao matumbo joto hasa baada ya kipa wao hodari Danijel Subasic kuumia misuli. Hat Sime Vrsaljko anasumbuliwa na goti licha ya kwamba Madaktari wamesema hali yake sio mbaya sana.

Vikosi vinavyotarajiwa.

England XI: Pickford, Walker, Stones, Maguire, Trippier, Henderson, Alli, Lingard, Young, Sterling, Kane

Croatia XI: Subasic, Vrsaljko, Lovren, Vida, Strinic, Rakitic, Modric, Rebic, Kramaric, Perisic, Mandzukic

Na Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here