Home Uncategorized Ronaldo naye huyu hapa na barua yake, aeleza kwanini anaondoka

Ronaldo naye huyu hapa na barua yake, aeleza kwanini anaondoka

14612
0
SHARE

Tumesikia kwa Real Madrid tayari na tumesikia kwa kila mtu, lakini Cristiano Ronaldo alikuwa kimya na sasa kwa mara ya kwanza Ronaldo ametoa yake ya moyoni baada ya Real Madrod kutoa taarifa yao.

“Kwa muda wote niliokuwa katika jiji la Madrid na kwenye timu hii inawezekana ikawa nyakati za furaha zaidi kwangu kuwahi kunitokea, ninasema asante kwa mji huu na kwa klabu hii

Ninashukuru kila mmoja kwa muliyonitendea japokuwa naamini sasa imefika wakati wa kufungua ukurasa mpya katika maisha yangu na mpira wangu na ndio maana nikaiomba klabu kuondoka

Ninaomba msamaha na ninaomba mashabiki wangu wote kunielewa katika jambo hili, imekuwa miaka 9 ya mafanikio sana, miaka 9 ya kipekee zaidi katika soka.

Nimefurahia sana nyakati zote nilizojitolea na kupambana hapa, nimefurahi sana maisha yangu na wachezaji na wafanyakazi wa timu hii na hakika siwezi kusahau.

Ninakumbuka nyakati nzuri ikiwemo kombe la Champions League mara 3 mfululizo na kubeba mara 4 katika misimu 5, huku nikifanikiwa kupata kiatu cha dhahabu mara 3.

Real Madrid imeuchukua moyo wangu na wafamilia yangu na ndio maana kwa hali ya kipekee zaidi ninasema tena asante kwa ushirikiano mlionipa.

Namshukuru raisi Perez, benchi la ufundi, madaktari, wachezaji na kila mtu, kwa miaka hii 9 nimefanikiwa kukutana na wachezaji bora zaidi nikiwa nao ndani ya klabu hii

Nimefikiria sana na naona sasa ni wakati wa kuondoka, lakini jezi ya Madrid na uwanja wa Bernabeu bado nitakuwa navyo kichwani, asanteni na kama nilivyosema miaka 9 iliyopita ninasema tena Halla Madrid”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here