Home Kimataifa 2009-2018 safari ya Cr7 ndani ya Real Madrid mwanzo hadi mwisho

2009-2018 safari ya Cr7 ndani ya Real Madrid mwanzo hadi mwisho

7709
0
SHARE

Ndani ya masaa 12 yaliyopita Cristiano Ronaldo amewaaaga mashabiki wa Madrid, Real Madrid wamemuaga Ronaldo na kumtakia kila la kheri na Juventus wamemkaribisha Cristiano Ronaldo, lakini tujikumbushe alivyotua Madrid na hadi anaondoka.

2009. Baada ya kushinda michuano ya Champions League, FA, EPL Cristiano hakuona sababu ya kuendelea kubaki United alijiunga na Real Madrid kwa ada ya £90m ikiwa usajili wa gharama zaidi kwa wakati huo.


29/ 8 /2009. Hii ilikuwa siku ya kwanza kwa Cristiano Ronaldo kuvaa uzi wa Real Madrid, ilikuwa mechi ya La Liga dhidi ya Deportivo La Coruna wakashinda mabao 3-2 huku Cr7 akifunga kwa mkwaju wa penati.

Akafunga mechi zote 4 za mwanzo kwa Madrid lakini October aliumia enka ikamuweka nje wiki 7, na wiki moja baada ya kurudi alipewa kadi nyekundu, pamoja na yote hayo Ronaldo akamaliza msimu na mabao 33(mashindano yote).

2010/2011, mambo yalianza kumnyookea akipewa jezi namba 7 baada ya Raul kuondoka Real Madrid na katika msimu huu kwa mara ya kwanza akafunga mabao 4 katika mechi moja, ilikuwa October 23 vs Racing Santander.

Msimu huu Ronaldo alifunga mabao 11 kwa siku 30 tu(mabao mengi zaidi ndani ya mwezi), akafunga hattrick 4 na msimu huu akaifikia rekodi yake ya mabao 42 kwa msimu mmoja na hiyo ikiwa November.

Lakini hadi mwisho wa msimu wa pili wa Cr7 ndani ya Madrid alifunga mabao 53 na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 40 La Liga msimu mmoja na akatwaa kiatu cha mfungaji bora.

2011/2012. Hapa ndio Ronaldo alifunga bao lake la 100 kwa Madrid na ilikuwa dhidi ya Barcelona, na bao lake la 100 La Liga akalifunga dhidi ya  Real Sociedad.

Msimu huu Cr7 alikuwa wa pili katika tuzo ya Ballon D’or lakini msimu huu akafunga mabao 60 kwa msimu mmoja akivunja rekodi yake ya msimu uliopita ya mabao 53 na hapa akawasaidia Madrid kubeba La Liga mara ya kwanza tangu ajiunge nao.

2012/2013. Hapa chokochoko za kuondoka Madrid zilianza baada ya kunukuliwa kwamba hana furaha na Madrid, lakini msimu huu ndio msimu wake wa kwanza kufunga hattrick akiwa na Madrid katika champions league,(vs Ajax).

Msimu huu akawa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi 6 mfululizo za El Clasico, akafanikiwa kubeba kombe la mfalme na Spanish Super Cup, msimu ukaisha akiwa na mabao 59.

Pia katika msimu huu ndio ambapo Cr7 kwa mara ya pili aliibuka kinara wa mabao Champions League akiwa na mabao 12 lakini Madrid wakaondolewa na Borussia Dortmund katika nusu fainali.

2013/2014. Hapa Ronaldo akaunganishwa na Gareth Bale wakaitengeneza BBC, Ronaldo anasema huu ndio msimh bora kwake kwani hadi mwishoni mwa November alifunga mara 32 katika mechi 22.

Akavunja rekodi ya Messi ya mabao 14 katika msimu mmoja katika Champions League, Real Madrid wakafanikiwa kubeba kombe lao la 10 la UEFA huku Cr7 akibeba Fifa Ballon d’or  yake ya kwanza akiwa na Madrid, akashinda mchezaji bora La Liga na bora Champions League.

2014/2015. Mechi 8 tu za mwanzo Cr7 alifunga mabao 15 La Liga, msimu huu alifunga hattrick yake ya 23 La Liga, akafunga bao lake la 200 La Liga na akamaliza msimu na mabao 61 katika michuano yote.

Akashinda kikombe cha klabu bingwa dunia katika msimu huu, na hapa akashinda tena tuzo ya FIFA Ballon D’Or akiwa mchezaji wa nne kuwahi kushinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo, akashinda kiatu cha dhahabu La Liga mara ya pili mfululizo na kiatu cha dhahabu Ulaya.

2015/2016.  Maisha ya Cr7 ndani ya Madrid yakazidi kumnyookea, msimu huu ndio akaweka rekodi ya mfungaji bora wa Madrid katika La Liga(mabao 230) na mfungaji bora muda wote wa Madrid (mabao 324).

Msimu huu akawa mchezaji wa kwanza kufunga mabao zaido ya 9 katika hatua ya makundi ya Champions League(mabao 11), lakini ni msimu huu ambao Cristiano aloshindwa kutetea tuzo yale ya FIFA Ballon D’or ikienda kwa Messi, lakini wakabeba tena Champions League ya 11, huku akipewa tuzo ya mchezajo bora wa Ulaya 

2016/2017. Alianza kwa majeruhi ambayo yalimkosesha katika michezo 2 ya kwanza ya Real Madrid ikiwemo mchezo wao wa fainali ya Uefa Super Cup vs Sevilla lakini msimu huu akasaini mkataba mpya na Real Madrid uliokuwa unamuweka hadi 2021.

Msimu huu akafunga bao lake la 500 kwa Real Madrid(vs Club America), huku hattrick aliyofunga dhidi ya Atletico ikimfanya kuwa kinara wa mabao wa Madrid Derby(mabao 18).

Akaisaidia Real Madrid kubeba klabu bingwa dunia akifunga hattrick kwenye fainali dhidi ya Kashima Antlers, akabeba Ballon D’or yake ya nne, tuzo ya mchezaji bora wa FIFA na kubwa kuliko akabeba ubingwa wa UEFA na Ureno bila kusahau Champions League.

Rekodi zinazidi kuandikwa kwenye daftari la Mreno, huu ndio msimu ambao aliisaidia Madrid kuwa klabu ya kwanza kufikisha mabao 5900 ya ligi, huku yeye akiwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 100 katika Champions League.

Msimu huu huu Cr7 aliweka rekodi kuwa nyota wa kwanza kufikisha mabao 50 katika hatua ya mtoano Champions League akifunga hattrick vs Atletico Madrid.

2017/2018. Mwanzo tu wa msimu aliisaidia Real Madrid kubeba kombe la mfalme akifunga moja ya bao wakati wakiifunga Barcelona kwa mabao 3-1 katika mchezo wa fainali, na msimu huu akafunga bao la 411 kwa Real Madrid.

Mwezi wa 10 mwaka jana alafanikiwa kubeba tuzo ya mchezaji bora wa FIFA kwa mara ya pili mfululizo na huku pia ukawa msimu ambao Cristiano Ronaldo akabeba tuzo yake ya 5 ya Ballon d’or.

Katika mchezo wao vs Atletico Madrid kwenye msimu huu Cristiano Ronaldo alifunga goli lake la 650, huku akiisaidia Madrid kutwaa kombe la Champions League la 3 mbele ya Liverpool mfululizo na akiibuka kinara wa mabao wa michuano hiyo kwa mara ya 6 akiwa na Real Madrid alimaliza na mabao 15.

Kwa ujumla akiwa na Real Madrid Cristiano Ronaldo ameichezea mechi 438 akafunga jumla ya mabao 450, assist 119, akabeba Champions League mara 4, La Liga 2, Copa Del Rey 2, tuzo za Ballon D’Or alibeba 4 na kiatu cha dhahabu mara 3.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here