Home Kimataifa Majina matatu mezani kwa Florentino Perez, nani kuvaa viatu vya Cristiano Ronaldo?

Majina matatu mezani kwa Florentino Perez, nani kuvaa viatu vya Cristiano Ronaldo?

18839
1
SHARE

Klabu kubwa kama Real Madrid linapokuja suala la usajili wa nyota wakubwa haiangaliwi tu kiwango cha nyota huyo uwanjani bali anatazamwa kama brand ambayo italeta faida ndani na nje ya uwanja.

Hii imekuwa ni desturi ya timu kubwa na tajiri katika siku za usoni kununua nyota ambao wanaibeba sura ya klabu kwa mvuto wa nje (matangazo, image ya mchezaji na mvuto kwa wawekezaji) na pia kiwango.

Cristiano Ronaldo ameondoka Real Madrid baada ya miaka 9 ya mafanikio ndani na nje ya uwanja, Florentino Perez ameridhia na sasa yuko sokoni rasmi kutafuta mtu mpya ambaye anaweza kwenda kuwa mfalme mpya Madrid.

Ndio anakwenda kuwa mfalme kwani kwa sasa Madrid wanabaki kuwa kama timu bila ya nyota mkubwa wa kumuangalia, tofauti na alipokuwa Ronaldo, au zama za Raul Gonzalez na hii sio sifa ya Madrid, Los Blancos ni lazima wawe na mtu au watu haswa wa kuitikisa dunia, ni nani sasa anakwenda kuvaa viatu vya Cr7.

Neymar. Kwa kipindi kirefu sasa tangu akiwa Barcelona amekuwa anahusishwa na uhamisho wa kwenda Real Madrid, Neymar alikimbia kivuli cha Messi Barcelona akajaribu kutengeneza ufalme wake PSG lakini ugumu unakuja kwa PSG kama timu haiwezi kukaa juu ya miamba ya Ulaya.

Inasemekana Neymar hakuwa na furaha PSG wakati wa kocha Unai Emery na hili lilianza kumfanya ajute kwenda Ufaransa, na jina la Real Madrid likaanza kutajwa.

Ameshatolewa World Cup na ndoto ya Ballon D’or mwaka huu inaonekana kufa, washauri wanamuambia namna pekee ya yeye kutwaa tuzo hii ni kuvaa viatu vya Real Madrid na huu unaonakena ndio wakati sahihi.

Utafiti wa shirika la CIES unaonesha Neymar wakati anajiunga na PSG alikuwa mchezaji mwenye ghali zaidi nje na ndani ya uwanja(hadi mwezi June tarehe 3) na hii ni wazi inaweza kuwa target namba 1 ya Perez kwa ajili ya biashara na mafanikio, huku Neymar mwenyewe anaweza vutiwa na usajili huu.

Kwa sasa duniani Neymar ndio mchezaji ambaye anazivutia kampuni nyingi kuliko mchezaji yeyote na uwezo uwanjani hilo halina shaka, sitashangaa Madrid akitunisha misuli yake ya pesa kwa kumtwaa Neymar.

Kylian Mbappe. Watu wanasema ni ngumu , lakini hakuna kinachoshindikana kwa Real Madrid wakikutaka wanakuchukua, wana nguvu ya pesa na historia yao kubwa inawafanya kutamaniwa na kila mchezaji.

Mbappe ana miaka 19 tu lakini moto anauonesha haujaonekana kwa kipindi kirefu kwa mchezaji mwenye umri kama wake, kiwango chake kombe la dunia si ajabu kikaanza kumuweka level za Messi na Cr7 katika Ballon D’Or.

Perez hawezi acha lulu ya namna hii iende hivi hivi, Mbappe mwenyewe anajua ni rahisi kuwa bora duniani ukiwa Real Madrid kuliko PSG na anataka kupitia njia za Role Model wake(Cristiano Ronaldo) kufikia mafanikio aliyoyapata.

Huwezi mfananisha Mbappe na Neymar katika biashara, wala huwezi linganisha uwezo wake na Cr7(ana safari ndefu) lakini huwezi kupepesa macho ukiulizwa nani anaonekana kuwa mrithi wa Messi na Ronaldo? Jina lake lazima liwepo.

Eden Hazard. Leo baada ya Cristiano kwenda Juventus, mashabiki wa Real Madrid walisikitika sana lakini mashabiki wa  Chelsea walishikwa na uoga mkubwa.

Eden Hazard, Real Madrid walimnyatia sana lakini baadaye wakaachana naye lakini sasa ni wazi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Madrid kuingia na nguvu zote kumtwaa Eden Hazard.

Katika wakati huu ambao Perez anahitaji mtu wa kuwaboost ndani na nje ya uwanja, kiwango cha Eden Hazard akiwa na Chelsea na Ubelgiji kinaweza kumfanya kuwa mtu sahihi kuvaa viatu vya Ronaldo.

Lakini pia sitashangaa endapo Real Madrid watafanya sajili mbili kubwa sana katika dirisha hili la usajili, tusubiri tuone nini Perez anakwenda kukifanya.

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here