Home Kimataifa Hayawi hayawi yamekuwa, Cr7 huyoo anakwenda Juventus

Hayawi hayawi yamekuwa, Cr7 huyoo anakwenda Juventus

10693
0
SHARE

Zilianza kama tetesi lakini hatimaye kila kukicha inaonekana kuwa ni kweli, Cristiano Ronaldo anaelekea Juventus rasmi baada ya vilabu vya Juventus na Real Madrid kukubaliana ada ya uhamisho. .

Uhamisho wake wa kuondoka Estadio Santiago Bernabeu unatarajiwa kutangazwa ndani ya masaa kadhaa kutoka sasa kwa mujibu wa MARCA.

Florentino Perez alijaribu kupindua meza kwa kuboresha mkataba wa Ronaldo lakini mchezaji alishaamua kuondoka na sasa amemruhusu kutimiza matakwa yake ya kujiunga na Juventus.

Kwa mujibu wa Jugones de La Sexta, Real Madrid wanatarajia kupokea cheque ya 100 million euro kutoka kwa Juventus jioni ua leo.

Wakati huo, Mwenyekiti wa Juventus  Andrea Agnelli leo asubuhi ameonekana uwanja wa ndege akielekea Ugiriki, mahala ambapo Ronaldo yupo na familia yake kwa ajili ya mapumziko – Agnelli alifunga safari hiyo baada ya kupewa ruksa ya Madrid ya kwenda kufanya mazungumzo na Ronaldo.

Cristiano mwenyewe anaonekana kuwa mkimya sana katika kipindi hiki na kuwa karibu zaidi na familia yake kwani katika siku za karibuni ameonekana akiwa na mtoto wake pamoja na mama wa watoto wake Georgina wakiwa mapumzikoni kusubiria nini kitatokea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here