Home Kimataifa Nusu fainali ya Ubelgiji vs Ufaransa katika namba

Nusu fainali ya Ubelgiji vs Ufaransa katika namba

7818
0
SHARE

9. Timu ya taifa ya Ubelgiji hadi sasa ina wachezaji 9 waliofunga mabao katika michuano ya kombe la dunia 2018, ni Ufaransa 1982 na Italia 2006 ndio timu pekee ambazo zimewazidi katika idadi ya wafungaji wengi kwa msimu mmoja(10).

6.Hii ni nusu fainali ya 6 kwa Wafaransa, wameshacheza nusu fainali ya 1958, 1982, 1986, 1998 na 2006, katika hizo ni nusu fainali 2 tu walifanikiwa kufudhu kwa hatua ya fainali (1998 na 2006).

73. Kwa ujumla timu hizi mbili zimewahi kukutana mara 74, katika mechi hizo walizokutana Ubelgiji walishinda michezo 30, Ufaransa wakashinda michezo 24 huku 19 kati ya hiyo ikawa suluhu.

2. Hii ni mara ya pili kwa Ubelgiji kucheza nusu fainali ya kombe la dunia, hawajawahi kupita katika hatua hii kwani nusi fainali yao ya mwisho mwaka 1986 walifungwa na Argentina, Diego Maradona akiweka zote.

7. Hii ni idadi ya mabao ambayo Antoine Griezman amefunga katika mechi sita za Ufaransa zilizopita katika hatua ya mtoano michuano ya Ulaya na kombe la dunia.

15. Hii ni idadi ya wachezaji wa Ubelgiji ambao walikuwepo mwaka 2014 katika michuano ya kombe la dunia, lakini 2018 tena wamerudi na timu yao ya taifa nchini Urusi.

7. Kama hufahamu tu ni kwamba Ubelgiji wameshatoa kipigo cha bao 7 mara mbili kwa Ufaransa, mara ya kwanza ilikuwa 1906 na mara ya pili ikawa 1911 lakini mechi zote hizi mbili zilikuwa za kirafiki.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here