Home Kimataifa Southgate na somo kwa Mourinho kuhusu Jesse Lingard

Southgate na somo kwa Mourinho kuhusu Jesse Lingard

9803
0
SHARE

Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia, nyota wa Manchester aunited Jesse Lingard alinukuliwa akisema anajiamini zaidi akiichezea timu ya taifa kuliko akiwa Manchester United, kauli ambayo iliibua hasira kwa mashabiki wa United.

Lakini siku chache baadae tukiwa tumebakiza michezo miwili kukamilisha kombe la dunia, Jesse Lingard anaonekana mtamu zaidi anavyotumiwa na Southgate tofauti na anavyotumiwa na Jose Mourinho.

Tangu Southgate amuweke nyota huyo na kumuamini kama kiungo hajawahi kuwa na utimilifu wa pasi chini ya asilimia 90 tangu michuano hiyo inaanza hadi leo.

Katika mchezo wa Uingereza vs Tunisia Lingard alikuwa wa moto sana na kuwahangaisha wa Tunisia na hadi mpira unakwisha #JLingz alikuea amepiga pasi kwa wastani wa 96.4%.

Mchezo kati ya Uingereza na Panama nao Lingard akaja akapiga pasi kwa wastani wa 94.3% huku akifunga bao bora zaidi kwa Waingereza katika michuano hii ya kombe la dunia 2018. Vs Colombia Lings alikuwa na wastani wa 90.6%.

Katika mchezo dhidi ya Sweden sasa Lingard alikokota mpira mara mbili zaidi ya mchezaji yeyote katika mchezo huo, alitoa assist ya bao la Dele Alli, ndiye mchezaji alipiga mashuti mengi zaidi na alikuwa na pasi 93.5%.

Kiujumla Jesse Lingard ana wastani wa 93.4% kwa mashindano yote kwa pasi timulifu na hii inamfanya kuwa namba mbili katika orodha ya viungo wenye wastani mzuri wa pasi timilifu kwa wachezaji ambao wameanza walau mechi tatu kombe la dunia.

Akiwa Uingereza Southgate amemuweka huru sana tofauti na United, na hili limemfanya kuwa mchezaji ambaye alicover uwanja kwa sehemu kubwa zaidi kwa wachezaji wa Uingereza katika mechi dhidi ya Colombia, Sweden na Tunisia.

Mechi dhidi ya Colombia kwa mfano, Lingard alikimbia kilomita 15.4 uwanjani na kuwa mchezaji ambaye amecover sehemu kubwa katika mashindano kwenye mechi moja, huku dhidi ya Sweden akicover 12.01km.

Tofauti na michezo iliyopita, katika mchezo ujao Uingereza wanakutana na midfilder pacha bora zaidi Urusi (Modric na Ractic), na hapa Southgate pamoja na mashabiki walioongezeka wa Lingard wanasubiri kuona nini atafanya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here