Home Kitaifa Simba yabadili gia kupata kocha wa viwango

Simba yabadili gia kupata kocha wa viwango

9924
0
SHARE

Uongozi wa Simba umesema unajipanga kuhakikisha unaboresha benchi la ufundi kwa kuwashirikisha wataalam wa soka na si kufanya mambo kwa mazoea.

Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah aameeleza namna walivyojipanga kwa ajili ya kupata kocha mwenye viwango.

“Simba inataka kubadikisha utaratibu wake wa kupata walimu, ili mwalimu awe mzuri ni lazima mwalimu huyo atafute kazi na afanyiwe interview. Tunao wataalam mbalimbali tunaweza kuwapa kazi ya kuwafanyia interview  hao makocha kuona kama wana-fit kwenye mfumo na soka letu”-Salim Abdallah.

“Tumekuwa tukichukua makocha wengi wakija hapa baada ya muda mfupi tunaona hawafai ni kwa sababu hatukushirikisha wataalam. Sisi viongozi tunaajiri walimu wa mpira wakati sisi si wataam katika eneo hilo.”

“Tutakuwa tukitangaza kazi, walim wanaoomba tunawakutanisha na wataalam ili wafanyiwe interview, ili tujaribu na mfumo huo hiyo ndiyo maana ya mabadiliko.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here