Home World Cup RUS 2018: Kama tulimzuia Messi, huyu Kane hatusumbui!

RUS 2018: Kama tulimzuia Messi, huyu Kane hatusumbui!

6827
0
SHARE

Croatia, dhidi ya England, hapatoshi.

Siku ya Jumatano kutakuwa na mchezo wa nusu fainali kati ya Croatia, dhidi ya England mchezo huu utaibua taswira kibao kwa mashabiki mbali mbali kokote duniani kutokana na nidhamu za timu hizi. hakuna mtu yoyote aliyekuwa akizipa nafasi hizi timu kufika hatua kama hii.

Ukiangalia hizi timu zinazokutana leo katika kama hi mara ya mwisho kucheza hatua kama hi ni miaka 20-28 walicheza tena kizazi cha miaka hiyo.ukiangalia England, mara ya mwisho kucheza hatua ngumu kama hii ilikuwa Mwaka 1990 kule nchini Italy, walitolewa kwa mkwaju ya penalt na Ujerumani 4-3 kikosi cha England kilikuwa kinaongozwa na nyota kadha akiwemo Peter Shilton, Gary Linker, na Chris Waddle, leo hi hawapo tunaona kabisa timu hi imepata wakati mgumu Sana wamekaa zaidi ya miaka 28 bila ya kufika hatua kama hii.

Croatia, mara ya mwisho kucheza hairs ngumu kama hi ilikuwa Mwaka 1998 kule nchini Ufaransa, mabao 2-1tena walipoteza mbele ya wenyeji wao kikosi cha Croatia, kilikuwa kinaongozwa na nyota kadhaa kama Slaven Billic, Niko Kovac, na Davor Sucker, imepita miaka 20 sasa tangu wachezea hatua kama hiyo.

Turudi katika fainali za kombe la dunia za Mwaka 2018, zinazoendelea hatua ya nusu fainali.
England, atacheza dhidi ya Croatia , mchezo huo unategemewa wa kuvutia zaidi kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya uwanja.
England, wamekuwa moja ya timu bora katika fainali za Mwaka huu wakiwa na nyota wadogo zaidi kuanzia umri wa miaka 20 mpaka 30 ukiangalia kabisa wachezaji wao wengi wanacheza ligi kuu ya England, wamekuwa wakitumia mfumo wa 3-5-2 umekuwa umewapa mafanikio zaidi katika ufungaji mpaka uanzishaji mashambulizi.

Mpaka sasa wamefunga mabao 11katika fainali hizi ikiwa inashika nafasi ya pili nyuma ya Belgium, wenye magoli 14. Mfumo huu umewapa faida kwa sababu wana wachezaji wenye speed na warefu zaidi ukiangalia katika safu yao ya ulinzi wachezaji Kama Jones Stones, na Maguire, wamekuwa wazuri kutumia mpira ya juu kufunga au mpira ya kutenga (set pieces). Katika magoli 11 magoli 8 wamefunga kwa njia hiyo tunaona kabisa wapo vizuri kwenye eneo hilo.

England, kuelekea mchezo wao wanahitaji kuwa na uimara katika eneo la kiungo kwa sababu hawana kiungo anayecheza namba 10 nyuma ya mshambuliaji ambaye ni mbunifu zaidi ya Sterling? sterling mzuri akitokea pembeni kwa sababu ndo namba yake halisi wanaenda kukutana na timu ambayo ipo vizuri eneo la kati wana viungo wabunifu kuna Modric na Rakitic je wataweza kuwazuia? jibu linawezekana kama watampa nafasi Eric Dier, kwa sababu Dier, ni mzuri kwenye kukaba na kufanya battle kutembea na Modric, kama wataweza hicho kitu basi watafanikiwa kupata ushindi Modric, ni mzuri kupiga pass za mwisho na kusukuma mashambulizi na hata kupiga mashuti.

Croatia, wamekuwa na timu bora eneo la kati na wamekuwa wanacheza mfumo wa 4-3-3 unaona kabisa eneo la kiungo Modric, Rakitic na Rebic, wamekuwa wabunifu zaidi kwenye kukaba na kupiga pass Modric, huwa anacheza free zaidi nyuma ya mashambuliaji mashambulizi yao huwa yananzia pembeni wakimtizama zaidi Ivan Perisic. Croatia, wasijisahau wakumbuke zaidi wanaenda kukubaliana na mshambuliaji bora kabisa duniani Harry Kane, mpaka ameshafunga mabao 6 Lovren, anamuelewa vizuri kwa sababu wote wanacheza ligi kuu England, nafikiri anahitaji kumpa mbinu beki mwenzake wa kati Alex Vida, kuhakikisha Kane aleti usumbufu.

kuna mtu kanitonya na kuniambia kuwa kama Croatia, wanahitaji kwenda fainali wamzuie Harry Kane kwa sababu ndo amekuwa kiu ya mafanikio zaidi watu wengi walishangaa kocha wa England, kumpa nahodha Harry Kane, anafanya kazi kubwa na ana hamasisha sana.

Kocha wa Croatia, amesema kuwa kama waliweza kumzuia Messi, basi na Harry Kane, linawezekana kumzuia amekuwa moja ya washambuliaji bora kabisa.

Na Aziz Mtambo!

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here