Home Kimataifa Rafael Nadal na Rodger Federer ni “BampaToBampa” Wimbledon, fainali ya 2008 yanukia

Rafael Nadal na Rodger Federer ni “BampaToBampa” Wimbledon, fainali ya 2008 yanukia

6867
0
SHARE

Baada ya timu ya taifa ya Hispania kuondolewa katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi, sasa walau Wahispania wamepata pa kujifichia na cha kuzungumzia.

Ni Rafael Nadal, tangu mwaka 2011 Mhispania huyo hajawahi kuingia katika robo fainali ya michuano ya Wimbledon, Nadal amefanikiwa kufudhu kwa robo fainali baada ya kumshinda Jiri Vesely kwa seti 6-3, 6-3, 6-4.

Kwa matokeo haya sasa Nadal anakwenda kukutana na kati ya Juan Martin Del Potro raia wa Argentina ama Gilles Simon raia wa Ufaransa katika robo fainali ya michuano hiyo.

Lakini habari kubwa baada ya Nadal kufudhu ni uwepo wa Rodger Federer kwenye michuano hiyo ambaye naye amefudhu kwa robo fainali baada ya kumchapa bila kupoteza seti Adrian Mannarino wa Ufaransa kwa seti 6-0, 7-5 na 6-4.

Mwaka 2008 wawili hawa walikutana katika hatua ya fainali na ndio fainali ambayo wataalamu wa hizi mambo wanasema ndio fainali bora kabisa ya mchezo wa tennis kuwahi kutokea na sasa inaonekana inaweza ikajirudia.

Kuanzia mwaka 2006 hadi 2011 Rafael Nadal alikuwa katika kiwango cha juu sana akifanikiwa kutinga fainali mara 5, lakini kuanzia 2011 alianza kuibuka kapa katika Wimbledon na majeruhi aliyopata 2009 yakitajwa kama chanzo cha kumshusha.

Hadi sasa Federer ameshashinda kwa seti 32 mfululizo na hii ina maanisha yuko nyuma ya seti 5 ya Nadal ambaye ameshinda seti 37 mfululizo, lakini wote hawajaifikia rekodi ya Bjorn Borg aliyewahi kushinda seti 41 mfululizo 1979-1981.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here