Home Kimataifa Luka Modric aichambua Uingereza na kueleza hofu kubwa kwake

Luka Modric aichambua Uingereza na kueleza hofu kubwa kwake

9944
0
SHARE

Croatia wamefudhu kwenda katika nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuwatoa Urusi, sasa Croatia watakutana na Uingereza katika nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia.

Kuelekea nusu fainali hiyo nahodha wa Croatia ambaye amewahi kuishi Uingereza wakati akiichezea Tottenham Hotspur Luka Modric ameelezea uwezo wa kikosi cha Uingereza na hofu yake kwao.

Modric anasema safari hii kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinaonekana kucheza kitimu sana na wameonekana kukamilika sana huku wakiwa hatari zaidi katika mipira ya adhabu,kona, mipira ya kutenga(set pieces).

Msimu huu timu ya taifa ya Uingereza ndio timu ambayo inaongoza zaidi kwa kufunga mipira ya kutenga wakiwa hadi sasa wamefunga mabao 8 kwa mipira hiyo, hii ni idadi kubwa ya set pieces kwa timu kufunga tangu 1966.

Modric amesema katika siku chache zilizobaki kuelekea mchezo wao dhidi ya Uingereza itawabidi wajifunze namna ya kuwazuia Waingereza wanapopiga mipira ya kona, adhabu na krosi.

Hadi sasa timu ya taifa ya Uingereza imefunga mabao 11 na kati ya hayo ni mabao 3 tu ambayo yamefungwa katika mazingira ya kawaida “open play”, hii inaonesha namna balaa la Waingereza  lilipo msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here