Home Kimataifa Henry atakitendea haki kibarua chake au kuzima ndoto za Wafaransa wenzake 65mil?

Henry atakitendea haki kibarua chake au kuzima ndoto za Wafaransa wenzake 65mil?

11047
0
SHARE

Kati ya malegend ambao wana heshima kubwa nchini Ufaransa ni Thiery Henry, amekuwa mhimili na mtu muhimu kwa Wafaransa katika soka akiwemo katika kikosi cha Ufaransa kilichotwaa kombe la dunia 1998, akiibuka kinara wa mabao wa Ufaransa kwa wakati huo.

Baada ya fainali ya kombe la dunia kwa Ufaransa 1998 walianza kuwa na nyakati mbaya kombe la dunia, mwaka 2002 pale Japan na Korea Henry na wenzake walikwenda na matumaini ya kutwaa ndoo lakini wakaondoka hatua ya makundi.

2006 tena Wafaransa wakaenda Ujerumani na matumani ya ndoo, Thiery Henry akafunga mabao 3 katika michuano hiyo wakafanikiwa kufika fainali lakini kipigo cha penati toka kwa Italia kikawazima.

Kabla ya kwenda South Africa 2010 moto ulianza kuwaka katika kambi ya timu ya taifa Ufaransa na wakaenda katika michuano wakiwa hawana team spirit, na kweli walipofika kwa mzee Madiba waliishia kwenye hatua ya makundi huku Henry akicheza dakika 53 tu.

Miaka 20 baadae Thiery Henry ni kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Ubelgiji ambayo inapewa nafasi kubwa kwenda fainali mara ya kwanza ya kombe la dunia na sio tu kwenda bali kulibeba kombe la dunia.

Lakini mtihani ni inapokuja njia ya Henry kuipeleka kombe la dunia, Henry anakutana na taifa lake alikozaliwa ambako watu wanamtazama yeye kama kioo cha soka lao lakini hii leo itabidi azibe macho na kuwatoa Wafaransa ili kwenda fainali.

Tangu mwaka 1998 baada ya Thiery Henry kutwaa kombe la dunia na Ufaransa hawajwahi kuwa na matumaini makubwa na kikosi chao kubeba kombe la dunia kama ilivyo kwa timu hii iliyoenda Urusi, Wafaransa wote wameungana kufanikisha hili lakini Henry itabidi atetee ugali wake kwa kuisaliti Ufaransa.

Lakini Henry atakuwa na mtihani mgumu sana kwani Ufaransa hawajawahi kuwaacha Ubelgiji, katika michezo 3 waliyokutana Ufarasna walishinda michezo (3-1 mwaka 1938, 4-2 mwaka 1986 na 5-0 michuano ya Ulaya mwaka 1984).

Lakini katika michezo mitatu ya mwisho ambayo timu hizi mbili zimekutana, Ubelgiji hawajawahi kupoteza hata mchezo mmoja huku ushindi unaokumbukwa zaidi kwa Wabelgiji mbele ya Wafaransa ni 4-3 mwaka 2015.

Hii itakuwa nusu fainali ya sita kwa Wafaransa lakini katika 5 zilizopita walifungwa 3 (1958, 1982 na 1986) na 2 walizoshinda zote Henry alikuwepo katika kikosi cha Ufaransa (mwaka 1998 na 2006).

Tayari striker wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud amemtumia salamu Thiery Henry na kumuambia “nitajaribu kukuonesha kwanini umechagua upande ambao sio sahihi” akimaaanisha watamuaonesha kwanini alifanya kosa kuwa upande wa pili.

Naye kocha wa Ufaransa Didier Dechamps akizungumza kuelekea mchezo wa leo amenukuliwa akisema “Henry ni adui wa soka la Ufaransa” akisisitiza kama ukienda mbali na nchi yako kuichezea klabu na ikaifunga klabu ya nchi yako huo ni “uadui wa soka la taifa” lakini kwa ngazi ya Henry ni uadui mkubwa zaidi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here