Home Kitaifa KMC imemsajili beki kutoka Stand United

KMC imemsajili beki kutoka Stand United

10101
0
SHARE

Ni mzaliwa wa Zanzibar aliyekuzwa katika kituo cha VIKOKOTONI JUNIOR CENTRE, timu ya GULION FC wakavutiwa na kipaji chake na kuamua kumsajili, akapata fursa ya kuiwakilisha wilaya ya MJINI katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17.

Baada ya kufanya vizuri katika klabu ya GULION FC, vilabu mbalimbali vya ligi kuu ya Tanzania Bara vikavutiwa na kijana huyu hatimaye akafanikiwa kutua STAND UNITED ya mjini Shinyanga na kuitumikia kwa kujituma, nguvu na maarifa mengi.

Kocha wa KMC FC Ndayiragije Ettiene alikibaini kipaji hicho na kuhitaji huduma ya kijana huyo, Mabibi na Mabwana beki wa kati ALI ALI rasmi amesajiliwa @kmcfc_official kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here