Home Kitaifa Haji Manara kuhusu tetesi za Wawa kutemwa Simba

Haji Manara kuhusu tetesi za Wawa kutemwa Simba

12158
0
SHARE

Haji Manara amekanusha taarifa zinazomhusisha beki Pascal Wawa kutemwa na uongozi wa Simba baada ya kutoridhishwa na kiwango alichokionesha kwenye mechi alizocheza kwenye mashindano ya Kagame Cup.

“Kuna taarifa zinaenea mitandaoni kwamba Simba inaachana na Wawa, hizi ni taarifa za uongo na kuzusha na kutaka kutuvuruga. Wawa hakucheza kwa kipindi kirefu, kajiunga na timu kafanya mazoezi siku mbili au tatu alikuwa anahitaji match fitness”-Haji Manara.

“Unapoangalia mechi za Simba za sasa, mashambulizi yote yanaanzishwa na Wawa. Kukosa speed kunasababishwa na kukosa match fitness ambayo haiwezi kupatikana kwa kukaa nje.”

“Kwa hiyo hizo ni taarifa za uongo, uongozi wa Simba una imani na Wawa na wachezaji wote waliopo pamoja na benchi la ufundi. Nakanusha taarifa hizo nawaomba wapenzi wa Simba waachane na porojo za mitandaoni.”

Wawa amesajiliwa na Simba hivi karibuni kwa ajili ya kuisaidia klabu hiyo kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa kwa msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here