Home Kimataifa Sweden wanaweza kuzuia “home coming” ya Waingereza hii leo au Harry Kane...

Sweden wanaweza kuzuia “home coming” ya Waingereza hii leo au Harry Kane awabebe

9405
0
SHARE

Ni mwaka ambao Waingereza wanaamini sana kwamba kikombe cha dunia kinarudi Uingereza mahali ambapo wanaamini ndio nyumba ya mpira, hii leo Uingereza wako uwanjani Samara Arena kuikabili Sweden.

Hii ni mara ya tisa katika michuano hii ya kombe la dunia ambapo Uingereza wanacheza robo fainali, lakini mara 7 kati ya hizo 9 waliishia robo fainali huku mara mbili tu 1966 na 1990 ndipo walipita hatua hii.

Ni tofauti kwa Sweden ambao wao wameingia robo fainali mara 4 , lakini hii ikiwa mara yao ya kwanza tangu 1994. Katika mara 4 ambazo Sweden wamecheza robo fainali wameshindwa kuvuka hatua hii mara moja tu, ilikuwa 1934 wakipigwa na Ujerumani.

Sweden wameshinda katika michezo yao miwili iliyopita ya kombe la dunia lakini hawajawahi kushinda michezo mitatu ya mfululizo katika michuano hiyo, mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa 1950 na 1958.

Upinzani baina ya timu hizi mbili ni mkubwa sana, mara 24 wameshakutana katika michuano tofauti na katika mara hizo 24 timu ya taifa Uingereza ilishinda mechi 8, Uingereza wakashinda 7 na mechi 9 wakasuluhu.

Mwaka 2002 walikutana katika kombe la dunia na kutoka suluhu ya bao 1-1 na kisha mwaka 2006 tena wakakutana na kusuluhu 2-2, katika mechi zote hizi Waingereza walitangulia kufunga na Sweden akachomoa.

Tishio kubwa kwa Uingereza ni matokeo yao na Sweden katika mechi za mashindano, katika mechi nane ambazo wamekutana katika mashindano, Sweden alishinda michezo mitano huku Uingereza akishinda mmoja na mechi mbili zikawa suluhu.


No Zlatan No Problem, Zlatan Ibrahimovich hayupo lakini Marcus Berg sio wa kumchukulia poa hata kidogo, hajafunga hadi sasa lakini ana shot 13 on target, ndio anaongoza kwa mashuti mengi bila kufunga goli na alikuwa mfungaji kinara wakati Sweden wakifudhu kombe la dunia.

Walinzi wa Sweden Mikael Lausting, Victor Lindelof, Andreas Granqvist nao wamekuwa wakiibeba sana Sweden katika mechi zao, hadi sasa wamefunga mabao 7 katika mabao 27 katika mechi zao zilizopita.

Andrea Granqvist, amekuwa akitajwa chachu ya mafanikio ya Sweden, amekuwa anaelewa wao hawapewi nafasi, na kuhusu Uingereza amesema “najua watu wasemacho, tukutane uwanjani”, huyu amekuwa nahodha haswa akiitia timu moyo na kukifanya kikosi kuwa chenye umoja wakati wote.

Hofu, Waingereza safari hii wanaonekana ni aina ya timu ambayo inapress sana kuanzia katika eneo lao la ulinzi mabeki wa pembeni (Ashley Young na Walker) na eneo la ulinzi la Sweden wako imara zaidi katikati na hii inaweza kuwa tatizo kwa Sweden.


Harry Kane, hili ni tishio la kila mtu Urusi ambaye haiungi mkono Uingereza, hajawahi kukosa goli. Katika mashuti 6 aliyopiga kwenye lango la wapinzani yote yalikwenda kimiani na hakuna Muingereza ambaye amewahi kufunga mabao mengi kumpita Kane.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here