Home World Cup RUS 2018: Croatia na Urusi hatoki mtu!

RUS 2018: Croatia na Urusi hatoki mtu!

9525
0
SHARE

Nimesoma andiko Natasha Singh akisema kwamba huenda wahindi wasiendelee tena kufuatilia kombe la dunia kwa wingi mwaka huu kwani wengi wao walikuwa mashabiki wakutupwa wa Brazil.

Timu ya Croatia na mwenyeji Russia leo wanaaumana ili kujua yupi anatimiza ndoto yake. Bila shaka wakati kombe la dunia halijaanza hakuna mtu akiyewahi kutabiri Urusi na Croatia eti zitafika hatua ya robo au mmoja wao atafika nusu fainali. Hakuna mtu aliyewaza haya. Tena ungesema haya basi ungechekwa. Ajabu leo hii Ujeruman, Brazil Argentina, Hispania na Ureno wapo kwa runinga.

Stanislav Cherchesov kocha mkuu wa Urusi na timu yake walikuwa na msimu mbovu sana hasa hasa mechi za kirafiki ambapo hawakushinda mchezo w kirafiki hata mmoja. Lakini sasa hivi Cherchesov anaonekana mkali wa mbinu za kupata matokeo. Makipa bora dunia kama De Gea na Neuer wamezidiwa ujanja hadi na mlinda lango wa Urusi Igor Akinfeev. Warussi hawawezi kumsahau mwokozi huyu aliyewatoa mdomoni mwa Hispania kwenye mikwaju ya penati.

Russia ni timu ngumu mno. Narudia ni timu ambayo wachezaji wake wamejitolea kupambana mpaka jasho la mwisho. Kwanza sura zao na mpira wanaocheza huku Raisi wao akiwa jukwaani ni wazi kwamba wanatisha. Dunia limeondokanana soka la majina au historia au vipaji. Sasa hivi ni nafasi, kujituma na kujiamini.

Tokea Urusi ishiriki kombe la dunia kama Urusi na sio umoja wa kisoshalisti haikuwahi kuvuka hatua ya makundi tokea mwaka 1994 ispokuwa mwaka huu.

Rekodi kubwa kwa Urusi ni mwaka 1966 iliposhika nafasi ya 4 katika michuano ya kombe la dunia wakati huo ikiwa kama Umoja wa nchi za kisoshalisti.

Kiungo wao anayefanya kazi chafu bwana Yuri Gazinsky anakwambia sisi tumeaminiwa na taifa tutashibdwa vipi kufanya maajabu. Ni taifa letu pekee lilituamini hakuna mtu mwingine aliyeamini kama tungewazuia Hispania. Hata wake zetu walikuwa na wasiwasi na sisi lakini kila kitu ni kujitoa.

Croati na Urusi wote wamefika hatua hii baada ya kushinda mikwaju ya penati Croatia vs Denmark na Urusi Vs Hispania

kwa mara ya kwanza Croatia kushiriki kombe la dunia ilikuwa miaka 20 iliyopita ambapo walimaliza nafasi ya 3. Kuna uwezekano mkubwa akina Luka Modric wakarudia yale yale ya 98. Kikosi chao hakina majina makubwa sana ila majina yenye uwezo yapo machache kama vile Modric, Ivan Perisic, Mario Mandzukic na Ivan Rakitic. Huenda wakarudia rekodi ya akina Davor Sucker Hakan Sukur na wenzao ya mwaka 1998.

Hofu kubwa ipo kwa Artem Dzyuba. Huyu jamaa ana urefu wa futi 6’7 amekuwa mtu hatari mno. Walinzi wa Croatia wanapaswa kuwa makini nae sana.

Uzuri wa Croatia wao wanacheza zaidi kitimu. Viungo wao wapo Imara sanna na wana uzoefu mkubwa. Bila shaka karata yao inakwenda kwa Croatia

Russia: Igor Akinfeev; Mario Fernandes, Ilya Kutepov, Sergey Ignashevich, Fedor Kudryashov; Roman Zobnin, Daler Kuzyaev; Aleksandr Samedov, Aleksandr Golovin, Denis Cheryshev; Artem Dzyuba

Croatia: Danijel Subasic; Sime Vrsaljko, Dejan Lovren, Domagoj Vida, Ivan Strinic; Ivan Rakitic, Marcelo Brozovic, Ante Rebic, Luka Modric, Ivan Perisic; Mario Mandzukic

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here