Home Kimataifa Ni Uingereza vs Croatia nusu fainali

Ni Uingereza vs Croatia nusu fainali

11347
0
SHARE

Harry Maguire aliwatanguliza Waingereza kwa bao la dakika ya na anakuwa mchezaji wa nne kuwahi kufunga bao katika michuano yake ya kwanza WC baada ya Rio Ferdinand, Alan Mullery na David Platt.


Kipindi cha pili dakika ya 59 Dele Alli(22) alifunga bao la pili na kuwa mchezaji wa pili kwa udogo kuwahi kuifungia Uingereza goli katika kombe la dunia baada ya Michael Owen kufanya hivyo 1998 akiwa na miaka 18.


Matokeo hayo ya Uingereza yaliipeleka katika nusu fainali kwa mara ya tatu, mwaka 1966 na 1990 zilikuwa mara mbili ambazo Waingereza walienda nusu fainali kabla ya mechi ya hii leo.

Katika robo fainali nyingine wenyeji wa michuano hii, timu ya taifa ya Urusi walijikuta wakiaga mashindano hii baada ya kuondolewa kwa mikwaju 5 kwa 4 ya penati.


Katika mchezo ambao ulikuwa mgumu sana Urusi walitangulia kwa bao la dakika ya 39 la Denis Cheryshev lakini Andrej Kramaric aliisawazishia Croatia, mpira ukaenda dakika 30 za nyongeza na Dimagoj Vida akaipa Croatia bao la pili kabla ya Mario Fernandea kusawazisha dakika ya 115.

Urusi inakuwa timu ya kwanza kuandaa michuano na kutolewa katika robo fainali(timu zilizofika robo), kwani katika fainali 5 zilizopita kombe la dunia ambazo wenyeji walifika robo fainali walifudhu kwenda nusu(Italia 1990, Ufaransa 98, Korea Kusini 2002, Ujerumani 2006 na Brazil 2014).


Matokeo ya leo yanaifanya Croatia kuwa timu ya pil kufudhu katika mechi mbili mfululizo za mtoano, timu ya kwanza kuwahi kufanya hivyo ilikuwa Argentina mwaka 1990 wakiitoa Yugoslavia na Italia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here