Home Kitaifa Mbeya City wametambulisha ‘uzi’ watakaoutumia 2018/19

Mbeya City wametambulisha ‘uzi’ watakaoutumia 2018/19

10375
0
SHARE

Kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara 2018/2019, klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya imezindua rasmi jezi zao mpya zitakazozitumikia katika michezo ya VPL na Kombe la FA msimu utakaoanza hivi karibuni.

Mbeya City imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya ligi kuu kutangaza au kuzindua jezi aina mbili tofauti kuelekea msimu ujao ambapo kutakuwa na jezi za nyumbani na ugenini zitakazotumika kwenye Ligi Kuu pekee na zitakuwepo nyingine zitakazotumika katika Kombe la FA pekee.

Jezi za Mbeya City zimetengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Sports Masters ambayo imekuwa ikiwadhamini kwa msimu wa pili sasa, meneja wa Sports Master Fadhili Nsemwa amethibitisha kuwa wamefanya hivyo ili kuboresha na kuleta mabadiliko.

“Kila mwaka tunakuja na kitu kipya Mbeya City inakuwa timu ya kwanza nchini kuwa na jezi maalum ya Kombe la FA pamoja na sare za makocha na msemaji wa timu”- Fadhili Nsemwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here