Home Kimataifa Tiketi za kumwaga kombe la dunia 2018

Tiketi za kumwaga kombe la dunia 2018

7775
0
SHARE

Katika pilika za hapa na pale kwenye miji tofauti ndani ya Russia Shaffih Dauda ameamua kufanya utafiti mdogo tu kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mechi za robo fainali.

Dauda ameamua kuingia kwenye utafiti huu kwa sababu kwa upande mmoja ni mhanga wa tiketi, aliwahi kushuhudia fainali ya UEFA Champions League kwenye Public Viewing lakini mpango wake ulikuwa ni kuzama ndani ya uwanja.

Hapa anatupa experience yake kuhusu tiketi wakati wa fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil na hali ikivyo sasa nchini Russia.

Ishu ya ulanguzi wa tiketi kwenye fainali za kombe la dunia safari hii kuna tofauti kubwa ukilinganisha na ilivyokuwa Brazil mwaka 2014.

Nilichogundua ni kwamba wakati huu tiketi hazina dili sana kwa zile ambazo zinalanguliwa kwa sababu nimeshuhudia tiketi za nusu fainali category 1 ambazo bei yake ni $750 wanaolangua wanauza $1000, tiketi za $250 watu wanataka $400 hadi $500 ambacho ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na ilivyokuwa Brazil.

Kwenye fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil, tiketi ya $300 watu walikuwa wanauziwa $2000 watu walikuwa wanaitafuta hadi kwa $3000.

Nimefanya uchunguzi nimegundua, kukosekana kwa baadhi ya timu katika hatua za mbele kumepelekea upatikanaji wa tiketi uwe mkubwa.

Kwa mfano mashabiki wa Argentina walinunua tiketi hadi za nusu fainali wakiamini timu yao itafika, lakini baada ya Argentina kutolewa wengi wanauza tiketi zao wanarejea nyumbani na hawaziuzi kwa faida wanauza ili warudishe angalau pesa zao.

Juzi nikiwa eneo la ‘Red Square’ nilikutana na waargentia wanne wanauza tiketi nane za nusu fainali itakayochezwa St Petersburg, bei ya tiketi ni $750 lakini wao walikuwa radhi kuuza $1200, $1000 na walipokuwa wanakaziwa sana waliuza hadi $750.

Ukiangalia fainali za 2014 zilizofanyika Brazil ukiachilia mbali kwamba ni nchi ambayo ni kichaa wa soka, angalia mataifa yaliyofika hatua ya robo fainali utakuta Brazil ilicheza vs Colombia, Argentina vs Ubelgiji, Costarica vs Uholanzi, Ujerumani na Ufaransa.

Uwepo wa timu nne kutoka Amerika ya Kusini (Brazil, Argentina, Costarica na Colombia) na timu nne za Ulaya (Ubelgiji, Uholanzi, Ujerumani na Ufaransa) ulifanya uhitaji wa tiketi uwe mkubwa kwa sababu ya timu zilizopo.

Safari hii timu kama Argentina, Colombia, Ujerumani hawapo ambao ndio wanunuzi wakubwa wa tiketi nchi zilizopo hata mashabiki wake hawakutarajia kama zitafika hatu hiyo (Sweden) ndiyo maana mzunguko wa tiketi ni mkubwa lakini hauna dili kama ilivyokuwa Brazil.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here